Wale wametengenezewa JEHANUM watateseka kwa KIU, kiu ambacho HAKITAWEZA kumalizika. Kumbuka vile tajiri katika jehanum alivyomsihi Ibrahimu “Luka 16:24” pia kumbuka ombi hili ndogo ILIKATALIWA. unaweza kufikiria vile tunaweza kukaa bila maji tunayoyafurahia kwa siku moja wacha milele na milele? Kuna jibu la kiu ya mwanadamu nayo ni Yesu anatukumbusha yeye ndiye maji ya uzima na anawasihi wote walio na kiu wamuendee YEYE na kunywa. "Yesu akajibu, "akamwambia, kama ungalijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiye, nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai." - Yohana 4:10 Je, umeshawai onja MAJI YA UZIMA ya Yesu Kristo? Je, UMEKAUKA na KUPOTEZA MAJI MWILINI? Usithubutu kuhatarisha kupoteza uzima wa milele kwa sababu ya KIU! Ijayo |