Wale wametengewa JEHANUM watateseka KUTENGWA MILELE. Watajua ya kwamba kuna shimo kuu katikati yao na Mungu. (Luka 16:26) Katika maisha yao hapa ulimwenguni alipata yote mazuri waliyoyapenda lakini sasa watatengwa na baraka za Mwenyezi Mungu MILELE NA MILELE. Umesikia watu wakifanya mzaha wakisema, “sitakua peke yangu jehanum, nitakua na rafiki zangu wote hapo”. Hawa watajua kwa kweli urafiki hauna dhamana katika moto na KUTESWA MILELE. Pia watateseka wakijua ya kwamba hawana uwezo katika hali hiyo yao. Hakutakua na nafasi ya pili ya kuchagua. Katika jehanum walijikuta,m itakua mahali mwao mwa kukaa milele na milele. Pale watakufa moyo na kujua ya kwamba watakaa hapo milele bila kuwa na nafasi ya kuokoka. Kumbuka maneno ya Ibrahimu kwa yule tajiri katika jehanum. “Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu .” – Luka 16:26 TAFADHALI CHAGUA LEO - NA SASA HIVI kwa wakati huu una nafasi Yesu anakutafuta uwe rafiki na Mwokozi wako. Waza moyoni Yesu ni rafiki yako na akija kwako na kugonga mlango na kila siku na siku unakataa kufungua. Mpaka siku atakapoenda. Usiendelee na kumkataa Yesu. Soma Waebrania 3:7-8 "Kwa hiyo, kama anenayo Roho Mtakatifu leo, kama mtaisikia sauti yake, Waebrania 3:7 Ifanye siku ya LEO siku YAKO ya kumpokea YESU kama BWANA na MWOKOZI wako Ijayo |