Kutakuwa wengine ambao watakuwa wafungwa wa jehanum, kwa sababu walikataa ukweli wa neno la upendo na utilivu inayohubiriwa na wengi leo


Wiki iliyopita barobaro mmoja kijana aliniuliza kanisa langu linafundisha na njia tofauti tofauti za kuingia mbinguni kwa sababu Mungu ni mmoja hata tukimwita Yesu, Buda, Alhah, …. Siunaweza kujua mafundisho kama yako ni ya akili duni?”


SI UKWELI HATA KAMWE.



Mungu alituambia sio akili duni lakini ni njia nyembamba.


"Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. 14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesoga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache." – Mathayo 7:13-14





Mungu atuonya tusiabudu MIUNGU MINGINE


“Usiwe na miungu mingine ila Mimi.” Kutoka 20:3


“Yaangalieni hayo yote niliyowambia; wala msitaje kabisa majina ya miungu mingine, wala yasisikizwekutoka kinywani mwako.” Kutoka 23:13


“Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa BWANA, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu. Kutoka 34:14:


Matumaini yetu ya milele ya wokovu ni nyembamba kwa sababu Yesu Kristo alisema hivyo. Ni kupitia Yesu Kristo ili mtu aweze kupata uzima wa milele.


" Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.” 1 Wakorintho 3:11


"Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.– Yohana 17:3

" Yesu akamwambia, "Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima, Mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi." - John 14:6 – Yohana 14:6


Kama kanisa lako lafundisha wokofu kwa NJIA NYINGINE nakusihi ujitoe kutoka katika mafundisho ya upotofu kabla hujachelewa jitafutie angano jipya na huende kwa kanisa inayofundisha BIBLIA PEKEE na siyo mafundisho ya watu. Kufuata njia yeyote na sio YESU KRISTO itakupeleka katika laana ya milele!


Ijayo