Katika maisha yako sasa unaweza kuwa umelala asubuhi jumapili (haya wako) juu ya gondoro yako nzuri. Kama haujamwamini Yesu Kristo na kuokoa moyo wako, wakati umekuwa mfupi sana dakika ifuatayo unaweza kuamuka katika jehanum, Jehanum si mahali pa kupumzika, Biblia imetuambia kutakuwa na mateso usiku na mchana milele na milele. " na yule Ibilisi, mwenye kuwadaganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele. – Ufunuo 20:10 Watu wataweza kuona, kusikia, kushika, kuona, na kunusa katika jehanum. Tunajua hivi kwasababu tajiri katika Luka 16:19-31, tajiri aliweza kumwona Abrahamu, aliweza kusikia sauti na pia kushika miali ya moto kwasababu ya maumivu ya moto. Alitamani kuonja maji. Ufunuo 21:8 Ujumbe wa furaha ni kwa wale wanao mwamini Yesu Kristo kwa sababu mahali maalum wametengenezewa. "Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi, kama kioo kiangavu. 22 Nami Sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana kondoo ndio Hekalu lake. 23 Na Mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-kondoo. 24 Na mataifa watatembea katika nuru yake, na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.25 Na Milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku. 26 Wao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake. 27 Na ndani yake haitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, mbali wale walio andikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo. "– Ufunuo 21:21-27 Jina lako limeandikwa katika kitabu cha Mwana-kondoo cha uzima, Kama huwezi kujibu ndio, kwa imani yako kwanini ungojee? Mwamini Bwana Yesu sasa
Ijayo |