Ni wazi utaishia katika jehanamu kama utakuwa mshirika wa Shetani. Biblia inasema Shetani atakuwa na hatia na adhabu milele baada ya kupoteza vita vya mwisho. Kulikua na vita Mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. - Ufunuo 12:7-9 Ni muhimu wewe binafsi kufanya uamuzi bila kumtegemea mwovu Shetani, kutegemea neno la Mungu ni kulinda maisha yako ya badaaye. Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa. Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako, ukashinde uingiapo katika hukumu.."– Warumi 3:4 Nakuomba wewe Mwenyezi Mungu unilinde na kuniongoza kwa sababu Shetani ni "baba wa uongo. " “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, asema yaliyo yake mwenyewe; kwasababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.”- Yohane 8:44 Wewe utafuata uongo? Au utafuata Yesu Kristo ndani ya moyo wako, usipompokea Yesu Kristo kama mwokozi wako ambaye anaokoa, utaingia katika jehanamu na kupata adhabu milele na milele. |