Jua kwa uhakika bila shaka ya kwamba hautaenda

Jehanum wakati utakapoaga Dunia

Mimi kwa kweli ni mtu mzuri, kwa hivyo nitaenda mbinguni, “SAWA, kwa hivyo nitende mambaya machache, lakini nitende mengi mazuri, kwa hivyo nitaenda mbinguni”.Mungu hatanipa Jehanum kwa sababu sihishi kulingana na Biblia. Nyakati zimepinduka!” geuka niwale tu watu wabaya kama wanajizi wa watoto na wauaji watakaotupwa Jehanum”.

Hizi zote kwa ujumla ni vijisababu, Lakini ukweli ni kwamba, huu wote ni uongo. Shetani, mtawala wa ulimwengu, anapanda mawazo haya kwa Akili zetu. Yeye, na mwengine yeyote ule anayefuata jia zake, ni Adui wa Mungu(1Petro 5:8). Shetani ni mdanganyifu na mara nyingi hujitokeza kama aliye mzuri (2 Wakorintho 11:14), lakini yeye ndiye anayedhibiti Akili zote ambazo si za Mungu, “ambao nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. (2 Wakirintho 4:4)

Ni uongo kuamini ya kwamba Mungu hajali kuhusu dhambi ndogo ama kama Jehanum imetegewa watu “walio wabaya”. Dhambi ya haina yeyote ile hututenganisha na Mungu, “hata uongo mdogo”. Kila mtu alitenda dhambi, na hakuna yeyote ule aliyekamilika kivyake kuingia mbinguni (Warumi 2:23). Kuingia mbinguni hakuhusiani ya kwamba eti mazuri yetu yanazidi mabaya yetu; tutakosa sote ikiwa hilo ndilo jambo. “Na ikiwa ni kwa rehema, Basi sio kulingana na matendo yetu tena; na ikiwa ni kwa matendo yetu, Basi, rehema sio rehema tena (Warumi 11:6) hakuna chochote kizuri tunachoweza kukitenda kutuwezesha kuingia mbinguni. (Tito 3:5) si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi, bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho mtakatifu.

“Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Mathayo 7:13. Hata ikiwa mwengine yeyote ule anaishi maisha ya dhambi pale utamaduni wa kumuamini Mungu haupo, Mungu hataruhusu hiyo. “Nanyi mlikuwa wafu kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yake atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi. Wefeso 2:1.2

Wakati Mungu aliumba ulimwengu, ulikuwa mkamilifu na mzuri, baadaye akaumba Adam na Hawa na akawapa kuchagua kati ya mema na mambaya, kwa hivyo chaguo lilikua lao, iwe kumfuata Mungu na kumutii. Lakini walijaribiwa na shetani kutomtii Mungu. Kwa hivyo wakatenda dhambi. Dhambi hii iliwatenganisha wao (na vizazi vyao vyote, sisi pia tukiwepo). Kutokuwa na ushirikiano mwema na Mungu. Yeye Mungu ni mkamilifu na mkatatifu na lazima haukumu dhambi. Kama wenye dhambi, hatungeweza kujipatanisha na Mungu kivyetu. Kwa hivyo Mungu alitengeneza njia inayoweza kutupatanisha na yeye mbinguni. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, mbali awe na uzima wa milele. (Yohana 3:16) Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. (Warumi 6:23) Yesu alizaliwa ili afe kwa ajili ya dhambi zetu ili tusipotee. Siku tatu baada ya kifo chake, alifufuka kutoka kaburini (Warumi 4:25) akijithimbitisha kushinda mauti, alipatanisha ule uhusiano mwema kati ya Mungu na binadamu ili tuwe na uhusiano mwema na yeye ikiwa tutamwaminini yeye..

“Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe Mungu wa pekee na wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. (Yohana 17:3) watu wengi wanamwamini Mungu, Hata shetani pia anamwamini. Lakini kupokea wokovu ni lazima kumgeukia Mungu, na kumwamini Yesu atende yale alisema atatenda. Yesu atatuokoa tu ikiwa tutamuomba atuokoe.” Warumi 10:13. Wokovu ni kuweka imani yako mikononi mwa Yesu.





Sasa, yeye alisema atakushika, unataka kumwamini?

Imani maana yake ni kujitolea, kumwamini Yesu kabisa, kuamini uwezo wa mikono ile iliyopigiliwa misumari. Nitaruka, na nining’inie ikiwezekana; hiyo sio kuamini. Kunayo dalili ya shaka kwa kutaka kuning’inia’ hiyo nikutegemea nguvu zako mwenyewe. Lakini kwa sasa itafakari kwa njia hii, Yesu alisema kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu. (1 Yohana 1:9). Je, wewe unaamini hivyo? Wakati unamuomba Yesu aokoe nafsi yako, yeye anaweza kufanya hivyo? Huu ndio wakati wa Imani, hayo yote ni ya Yesu kutimiza yale aliyoyahahidi kutimiza, yote yako kwa uwezo wake, juu ya ukweli wa neno lake liwe kweli.

Wokovu huu kutoka kwa Mungu hutokana na imani ndani ya Yesu Kristo kwa wale wote wanaoamini. Hakuna tofauti!!(Warumi 3:22). Biblia inafundisha ya kwamba, hakuna njia ingine yeyote ile ya wokovu ila tu, kupitia kwa Kristo. Yesu alisema katika Yohana 14:6, Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima, mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Yesu pekee ndiye njia ya wokovu, sababu ni kwamba yeye pekee ndiye anaweza kulipia hukumu ya dhambi Warumi 6:23. Hakuna ndini ingine kwa undani ama ubaya wa dhambi na matokeo yake. Hakuna dini yeyote ile yupenana malipo ya dhambi ila tu ile Yesu anapeana. Sio hata mwanzilishi wa dini yeyote ile ambaye Mungu alikuwa mtu. (Yohana 1:1,14) – Njia ya pekee ile ingetumika kulipia deni hii kubwa. Yesu ilikuwa ni lazima awe Mungu, ili alipe deni letu. Yesu ilikuwa ni lazima awe ni binadamu ili afe. Wokovu hupatikana tu kwa imani ndani ya Yesu Kristo! Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. Matemdo ya mitume 4:12

Kwa hivyo, turudi nyuma “naweza kujua aje ya kwamba nitaenda Jehanum wakati nikifa?” Jibu ni hii. Wakamwambia, mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako (Matendo ya mitume 16:31) Bali wote wliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake (Yohana 1:12) unaweza kupokea uzima wa milele kama zawadi ya Mungu BILA malipo.

Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. (Warumi 6:23) Unaweza kuishi maisha ya milele na Yesu mbinguni kwa sababu alihaidi . Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu, ili nilipo mimi, nanyi muwepo (Yohana 14:3)

Ndio, ni rahisi! Huwezi kupata msamaha toka kwa Mungu. Huwezi kulipia msamaha wako toka kwa Mungu. Unaweza ku upokea tu, kwa imani, kupitia neema na huruma za Mungu. Kama unataka kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi wako na kupokea msamaha toka kwa Mungu, hapa kuna ombi unalo weza kuomba. Kwa kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haiwezi kukuokoa. Ni kwa kumwamini Yesu Kristo pekee ndiko kutaleta msamaha wa dhambi. Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kwa kumshukuru kwa kukupea msamaha.

“Mungu, najua ya kwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu na nina weka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu/ya ajabu na kwa msamaha! Amina.”



HOME




AMAZING GRACE BIBLE INSTITUTE