UKWELI WA JEHANAMU


“katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake"
— 2 Wathesalonike 1:8-9

Watu wengi leo hawaamini kana kuna mahali paitwao jehanamu panaowaka moto mkubwa (ufunuo 21:8) wanaokufa bila Yesu uenda kutezwa milele. Hofu ni kwamba kuna watu wanaogeuza maandiko kwa malengo ya kwamba jehanamu siyo kama vile Biblia inavyofunza, kama ni mahali panapowaka moto na matezo mengi.

Biblia iko na ushuhunda wa kutosha kuonyesha kwamba jehanamu ni mahali pa matezo, ambapo wanaokufa bila Yesu wanahukumiwa kwa matezo na gadhabu ya Mungu (2 Wathesalonike 1:8, 9).

Hapa kuna maandiko ya kufikiria

Hesabu 26:10
nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza pamoja na Kora, mkutano huo ulipokufa; wakati moto ulipowateketeza watu mia mbili na hamsini, nao wakawa ishara.
Kora na waliompinga Musa walimezwa kwenye jehanamu ya chini.

Zaburi 9:17

Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.
Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu. Kwa uangalifu jehanamu hapa haimaanishi kaburi kama vile kiujinga wengine ufunza. Kwa vile kama jehanamu ingemaanisha kaburi, basi wenye haki uenda wapi? Biblia inafunza wenye haki na wasiohaki na wasio haki hawaendi mahali pamoja. Wasio haki utupwa jehanamu na walio haki kwa uzima wa milele.

Zaburi 139:8

Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
Hii ni kutofautisha mbinguni na jehanamu, siyo kati ya mbingu na kaburi. Angalia hili, nikitengeneza kitanda change jehanamu. Yeyote anayekwenda jehanamu uchagua kwa kumkataa Yesu kama mwokozi. Ni wasio haki utengeneza vitanda vyao jehanamu. Hakuna mwenye dhambi huenda mbingu. Karama ya uzima wa milele upeanwa bure kupitia kwa imani ndani ya Yesu Kristo. ( Yoana 14:6, Matendo 10::43, Ufunuo 22:17).

Isaya 5:14

wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo.”
Haingemaanisha chochote kama tu jehanamu ingemaanisha kaburi. Ingekuwa na haja gani kwa kuwalaani wenye dhambi kama ni mahali pamoja wenye haki pia huenda? Kwa kweli jehanamu ni mahali pa wenye dhambi wanapokufa kwa dhambi zao. Wenye haki uenda mbinguni kuwa na Bwana (2 Wakorintho 5:8).

Ezekieli 31:16

“Niliwatetemesha mataifa kwa mshindo wa kuanguka kwake, hapo nilipomtupa chini mpaka kuzimu, pamoja nao washukao shimoni; na miti yote ya Adeni, miti iliyo miteule na iliyo mizuri ya Lebanoni, yote inywayo maji, ilifarijika pande za chini za nchi.
Kwa kweli maandiko yanaonyesha jehanamu ni zaidi ya kaburi. Biblia inazungumzia kuhusu kushuka kwa shimo. Inazungumza pia kuhusu kutupwa jehanamu ambapo inaonyesha hukumu kutoka kwa Mungu mtakatifu. Kama jehanamu inamaanisha kaburi kama Mormons, Mashahidi wa Jehova na Manabii wengine wa uongo vile wanavyofunza, basi Mungu angesema weinye haki watatupwa jehanamu pia. Lakini Biblia haijasema hivyo kamwe. Ni wasio haki pekee watatupwa jehanamu. Shimo isiyo na mwisho mahali shetani hitwa malaika wa shimo isiyo na mwisho (Ufunuo 9:11).

Mathayo 5:28-29

“lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.”
Bibilia inafunza wazi kwamba wasio haki wote wameisha hukumiwa kwenda jehanamu. Kama jehanamu kwa uraisi inamaanisha kaburi, basi kungekuwa na hofu gani kuhusu kuzini, kulewa, kubaka, kuna kutotumia madawa ya kulevya na kufanya dhambi zingine zozote? Hakuna lingekuwa. Kama hakuna mahali pa mateso ya milele, basi hakuna haki inayotendeka kwa wote wafanyao maovu katika uliwmengu huu. Basi kuna faida gani ya kuwa mwenye haki? Kama kuna imani ya kwamba Biblia hi neno la Mungu, basi inafaa kuamini ya kwamba jehanamu ni mahali pa kilio na matezo panaowaka miale ya moto, mahali waovu wanaotezwa kutokana na matendo yao kinyume na mapenzi ya Mungu mtakatifu.

Mathayo 16:18

“Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”
Hili ni andiko la maana sana. Neno milango inaonyesha mapitio ya kwenda kuzimu (Jehanamu). Hakika anayekufa kwa dhambi zake bila Yesu amepotea milele na milele. Hakuna nafasi ya pili mara roho inapo ondoka ulimwenguni humu. Hakuna mahali paitwao ‘Purgatory’ na hakuna maombi ama mchango wa kanisa uanoweza kuondoa hau kupumguza gadhabu ya Mungu kwa wanaokufa bila Yesu Kristo.
Andiko hili linafunza adui mkubwa wa kanisa ni shetani na nguvu za kuzimu. Tunaweza kuona ushuhuda huu katika Waefeso: 6:12. Vita vyetu sio vya mwili na damu (ubinadamu) bali ni vya mautawala, nguvu na nguvu za giza kwa kiwango cha juu (Milango ya kuzimu).

Matthew 23:15…

“Woe unto you, scribes and Pharisees, hypocrites! for ye compass sea and land to make one proselyte, and when he is made, ye make him twofold more the child of hell than yourselves.”
The Bible speaks of being "a child of Hell." Matthew 5:9 speaks of the "children of God." Galatians 3:26 wonderfully states, "For ye are all the children of God by faith in Christ Jesus." Amen! Jesus called the scribes and Pharisees the children of Hell.

Mathayo 23:15

“Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.”
Biblia inazungumizia kuwa mwana wa jehanamu. Mathayo 5:9 inazungumzia kuhusu wana wa Mungu Wagalatia 3:26 “Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.” Yesu aliwaita makuani na Mafarisayo wana wa jehanamu. Amina! Yesu aliwaita waandishi na Mafarisayo wana wa Jahannam.

Marko 9:45-46

“Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.”
Biblia inafunza dhambi za kibinafsi ndio chanzo cha sababu za wenye dhambi kutokuja kwa Yesu na kuokolewa. (yoana 3:20). Tunasoma kwa maandiko ya kwamba moto wa jehanamu hautaweza kuzimika. “worm” asiyekufa inaonyesha nia ya mmoja ile itakaowakula milele. Sehemu baya ya jehanamu sio miale ya moto na mateso, itakuwa ikijua kwa moyo, Yesu alikulipia deni akapenda dhambi zako na kukataa kuja kwa Yesu uokolewe. Kwa kufafanua sio mtu awache dhambi hili aokolewe, lakini ni kupenda dhambi inayomzuia kuja kwa Yesu, mpaka matendo yake yajaribiwe (Yohana 3:20). Yesu alisema kwa Yohana 5:40, “Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima”. Kuokolewa ni sharti mtu akubali ni mwenye dhambi mbele za Mungu asiyetii neno lake takatifu (Warumi 3:19). Watu wengi hawaa nia ya kutubu. Bali wanachagua kuendelea kukana wakitoa sababu kwa dhambi zao. Mungu anatuitaji tukubali maovu yetu mbele zake, na kutafuta msamaha kupitia kwa mwanaye Yesu Kristo.

Luka 10:15

“Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu.” Yesu alitabiri hukumu na ukawakalia wazi haki wa Capernaum. Ni muhimu kuona ya kwamba Biblia inaendelea kusema “kutupwa chini jehanamu”. Inayo onyesha gadhabu kwa mkono wa Mungu kuhusu hukumu. Zaburi 7:11 inaonyesha ghadhabu ya Mungu kwa wasio haki kila siku. Pia twaona jehanamu ni zaidi ya mfano. Ijapokuwa maisha ya mmoja inaweza kuonekana kama jehanamu duniani, haiwezi kufananishwa na mateso na kuchomeka na moto wa milele.

Luka 12:5

Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo.
Hili andiko inashuhudia mauti ya pili inaotajwa kwenye ufunuo 21:18. Wanadamu wanaweza kutuua mara moja, lakini Mungu anaweza kutuua milele jehanamu. Andiko hili halingekuwa na maana yeyote kama jehanamu inamaanisha kaburi ama mahali pasipo na mateso. Ni hofu gani ingekuwa?

Luka 16:23

“Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.”
Kwa kuangazia maandiko yote nimezungumza na ninyi kuhusu ukweli wa jehanamu. Nani anaweza kuzungumza kwa hakika ya kwamba Luka 16:19-31 ni fumbo tu? Yesu hakusema ni fumbo. Yesu hakutumia maneno spesheli katika fumbo, lakini anazungumza kuhusu Lazaro na Ibrahim katika kifungu hiki cha maandiko. Ni wazi sio fumbo, na kama hi fumbo Yesu alikuwa anataka kueleza nini? Ingekuwa inaitilafiana kwa Yesu kuzungumzia kuhusu jehanamu kama sio mahali pa matezo na miale ya moto kama haingekuwa hivyo. Fikiia maneno ya Yesu kwenye Yohana 14:2. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Yesu alikuwa mtu wa neno lake. Alimaanisha kile alisema na alisema kile alimaanisha, jehanamu ni mahlai pa mateso au moto.

Yakobo 3:6

“Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.”
Again we find a Biblical reference to "fire of Hell."

Waraka wa Pili wa Petro 2:4…

Waraka wa Pili wa Petro 2:4… “Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaashilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;
Kama jehanamu ni kaburi tu, basi Mungu angeweza namna gani kuwatupa malaika walioasi jehanamu (Mgiriki Taturus)? Malaika hawafi kama binadamu. Hauwezi kuwazika futi sita chini. Tunasoma hawa malaika walioasi (mapepo). Wameifadhiwa kwenye pingu za giza wakigojea hukumu. Kuna maneno matatau ya Ugiribi kwa lugha ya Kiingereza yanayo maanisha ‘jehanamu’ leo. Mauti, kuzimu na ‘Tartarus’ kuzimu ni ziwa la moto (Ufunuo 2o:11-15). “Tarturus” ni mahali spesheli mapepo wamefungiwa wakigojea hukumu. Mauti ni mahali wapotofu wenye dhambi huenda wakifa (Mahali pa matezo ya moto, matezo na kutezeka).

Ufunuo 1:18…

“Na aliye hai; name nalikuwa nimekufa na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo fungu za mauti, na za kuzimu.
Hapa tunaona mauti na kuzimu ni vitu mbili tofauti. Natilia mkazo mbingu na kuzimu maana haya ni maeneo ya kweli na haya ndio majina yao. Kama jehanamu ni kaburi, basi hapangekuwa tofauti katika kifo na mauti.

Ufunuo 20:13-15…

Ufunuo 20:13-15… “Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.

Unawezaje kubishana na Biblia kuhusu “mauti ya pili”? Hakika kuna hukumu baada ya kaburi. Biblia inafunza wapotofu wenye dhambi watasimama kwenye majaribio na kutpwa kwenye ziwa la moto kulingana na matendo yao. Pia biblia inafunza mauti na kuzimu zilitupwa kwneye ziwa la moto “jehamanu”. Hii inaonyesha ya kwmaba mengi kuliko kaburi. Neno la Kiebrania Seoli ni, angano la kale sawa na mauti katika angano jipya jehanamu, Seoli haimaanishi kabisa kaburi. Inaweza kumaanisha yote na iko hivyo. Zaburi 9:17 ni mfano kamilifu.
“Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.” Hakika hii inamaanisha mengi kuliko kaburi, kwa maana hapo ndipo hata wenye haki wngeenda. Hainge maanisha chochote. Tafsiri kamili ni kwmaba wasiohaki na wote wanao msaahu Mungu watatezwa milele.

Biblia inaushuhuda wa kutosha unaonyesha jehanamu ni mahali pawakao moto. Wale watu wanaodharau na kukana kuweko kwa jehanamu iwakao moto wanamwita Mungu muongo. Aidha uamini Biblia ni neno la Mungu ama ukatae. Hakuna mahali pa katikati. “Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo, ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu. Watu hao ndio waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho.” (Yuda 1:17-19)

AMAZING GRACE BIBLE INSTITUTE