Kweli kuna jehanamu ya milele?
 

Ezekieli 18:20-27: Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake. Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa. Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi. Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi? Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa. Lakini ninyi mwasema, Njia ya Bwana si sawa. Sikilizeni sasa, Enyi nyumba ya Israeli; Je! Njia yangu siyo iliyo sawa? Njia zenu sizo zisizo sawa? Mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, akafa katika uovu huo; katika uovu wake alioutenda atakufa. Tena, mtu mwovu atakapoghairi, na kuuacha uovu wake alioutenda, na kutenda yaliyo halali na haki, ataponya roho yake, nayo itakuwa hai.

Kama mungu amekuwa wa huruma kwa mwanadamu kwa kutoa nafasi hili aokolewe kupitia kwa Yesu Kristo, hili apate kuishi katika furaha ya milele, je ingekuwa kitu cha maana kisheria hau haki zake kuto wahukumu wanaodharau karama hiyo ya wokovu?

Tunaamini kwa mwanga mkubwa vile Mungu anavyosema kwenye Ezekieli 18, kama hatawahukumu wasiohaki na itakuwa kitu cha maana, Mungu anawabariki waliohaki na kuwahukumu wasiohaki. Haitakuwa haki kwa mungu kuwabaraiki waliohaki na kutowahukumu wasiohaki.

Mungu, anasema (kifungu cha 25) ya kwamba mapito ya mwenye dhambi ni mabaya. Ni kwa nini? Ni kwa sababu badala ya wakubali na kuchukua njukumu kwa maovu yao, utaka kuwalaumu wengine na kutaka kuepuka hukumu kulingana na maovu yao.

Mungu anasema kama mwenye haki atawacha haki na kufanya maovu atafa, na kama mwenye dhambi atawachana na uovu, bila shaka hatakufa, bali ataishi (Mstari wa 27), swala hili kwa mara nyingine, njia zangu sio nzuri nyumba ya Israeli baya, (Mstari 29). Jibu lake ni ndio. Lakini njia zao zilikuwa baya. Mungu hawaheshimu wanadamu. Kila kitu umtengemea mwanadamu waliohaki wataokolewa na wasiohaki watahukumiwa.

Kama mwenye haki huishi na kufa kwa haki zake, haitakuwa haki kwa wasiohaki kufurahia baraka hizo. Kama imekubaliwa kuishi kwa maovu, basi wapi sheria ya Mungu: Mungu ni mwenye haki na huwahukumu wasiohaki

Kwa hivyo mahali pa hukumu sio mahali pasiofaa, hao bila sababu, bali ni mahali pa mapenzi na haki za Mungu. Paulo anasema 2 Wathesalonike 1:6-10 Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi; na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake; yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu). ukweli Mungu atalipisha kwa matezo kama vile Mungu mwenye haki uwabariki wenye haki.

Kuna mafunzo mengi yanayofundisha ya kwamba kuna mahali pa kukumu. Mathayo 5:22.10:28.13:41,46, Marko 9:42-48, Ufunuo 20:15, 21:8. Ushahidi ungefunja nguvu zilizoko kwenye funzo hili, sema ‘jehanamu’ Ni mahali paliokuwa nje ya Jerusalemu pa kutupa taka na kuzichoma. Hakuna ushahidi kwa yeyote kutupwa kwenye hiki kifuli (shimo) kama njia ya kuhukumiwa ama kutezwa. Yesu aliweza kuzungumza kwa kiwango cha juu kuhusu hukumu na matezo. Washaidi hawaamini na watu wa kimwili kwa urahisi hawamwamini Yesu na upinga (udharau) anayosema.

2 Petro 3:9 “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.” Lakini wote waokoke (1 Timotheo 2:4) na wafanye kila kitu kuwaokoa wote. Lakini anawacha njukumu (uamusi) kwenye mikono ya mwanadamu. Hakuna yeyote anayelazimishwa kutii, bali, wote wako na njukumu ya uamuzi. Haiwezekani kuondoa maandiko yanayofunza kuhusu jehenamu, kama vile haiwezekani kuyaondoa maandiko yanayofunza kuhusu nyumbani mbinguni. Tunatakiwa kujifunza jinsi ya kutokwenda huko kuliko tutoamini kuwepo kwake.

Yesu anasema: Mathayo 25:46 “Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.” Ujumbe huu unajieleza wenyewe. Funzo liko wazi. Kutakuwa na matezo ya milele kwa wasiotii na uzima wa milele kwa wanaotii. Kama hakuna matezo, hakuna furaha. Kama neno umilele, imefunzwa kwa wasiotii, inafaa pia kufunzwa kwa wanaotii.

Wanasema “mashahidi” na miundo mingine ni nani ‘ataharibiwa’ wamejiweka kwa sehemu ya Mathayo 10:28 inaosema Mungu anaweza kuaribu mwili na nafsi jehanamu. Lakini kwanza neno aribu haimaanishi kuvunja ama kuangamiza kabisa kwa mtu, lakini ni kuvunja kwa hali sawa. (Anavyosema Muyunani Lexicous). Ya pili Yesu anasema kuvunja huku ni zaidi ya kifo na usiwaongope wanaoua mwili lakini hawawezi kuua roho (nafsi).

Kama wasiotii wataaribiwa kabisa, maana wasiishi tena, basi hii haitakuwa hukumu ya milele.

Kumbuka ya kwamba watakaohukumiwa sio tu wauaji au, wezi bali ni wale wasiomjua Mungu na wasiotii injili. 2Wathesalonike 1:7-9) Watu wasio na mawazo mema; Matedo. 10: 12, 22, inafunza juu ya mtu mkubwa ambaye hakuwa ameokoka. Alipoisikia injili aliokoka (Mstari 33 – 43, 48). Yesu anasema mmoja amwamini, tubu dhambi (Lk: 13,3,5) Kiri (Mathayo: 10:32,33. Ubatizwe kwa ondoleo la dhambi. Mko 16:6. Matendo. 2:38 na uwe mwaminifu hadi kufa na nitakupa taji la uzima wa milele (Ufunuo 2:10).

Wasioamini na watu wa kimwili wanataka kuondoa mafundisho kuhusu jehanamu. (Hukumu ya milele). Wanaongea kuhusu upendo wa Mungu, bali hawamjui Mungu ama kulielewa neno upendo. Wanaongea kuhusu mwana kondoo wa Mungu na kutojali gadhabu zao. Ufunuo 6:16 “wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.”

Wengi wanaamini Mungu wa angano la kale ni mkali na Mungu wa angano jipya ni mpole. Lakini hii si kweli na kibiblia haiko hivyo. Kwa kuongezea, tunasoma hukumu ya milele kwenye anngano jipya. Ni Kristo sio Musa anayesema kuhusu moto wa milele hauzimiki. Wale wanaoliamini Biblia wanaamini pia mafunzo kuhusu hukumu wa milele.

 

MATEZO YA JEHANAMU

Mafunzo Kuhusu Jehanamu ni moja wapo ya mafunzo yanayofunzwa kwa maandiko. Jehanamu ikitajwa leo inachukuliwa kama utunzi, na kama wazo hili la jehanamu ni la kale na kwamba ni wale wanaofunza wanaamini mahali kama hapo pako. Hili si ngumu kuelewa. Mwanadamu wa kawaida huchukia wazo la kutoa hesabu la maisha yake mbele za Mungu mtakatifu, yeye (mwanadamu wa kawaida), hupenda dhambi na hataki kuishi bila dhambi. Akili zake hazimkatazi kuona ukweli wa jehanamu. Mwanadamu uishi maisha yale akifikiria ya kwamba akifunza yaliyo gumu kwake yatatoweka. Wacha wanadamu waishi vile wapendavyo kwa uaminifu ya kwamba pingamizi la wajinga yatafunja ukweli wa jehanamu.

Kuaribiwa jehanamu ni kwa wale wanaamini Biblia ni ya ukweli wanaweza kusimama na kuongea. Kutafakari matezo ya jehanamu ni moja wapo ya mambo unayofaa kufikiria kila siku katika maisha haya. Ezekieli 33:4 “basi mtu awaye yote aisikiaye sauti ya tarumbeta, wala haonywi, upanga ukija na kumwondoa, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.”

Kwa nini yeyote ajali kuhusu jehanamu? Kwa nini uchukue wakati ukisoma kuhusu jehanamu? Kuna sababu wa kadha zinazoonyesha umuhimu kwa nini ufanye hivyo.

Kuusikia ufunjaji wa jehanamu utigiza nafsi na kuamusha ulizi usio wa kweli.

Kulijua jehanamu usaidia mwanadamu kuepuka njia zake za dhambi. Wenye dhambi ushauriwa wasitende dhambi wakati wote wanaokumbushwa mara kwa mara matezo ya jehanamu.

Kuyajua matezo ya jehanamu uwasaidia wanaofikiria wameokoka kwa kumwamini Yesu Kristo na kanuni za injili, bali hawajaokoka na wanatembea kwenye barabara ya kuwaelekeza jehanamu, bila kujua.

Kwa nini watu hawaongopi jehanamu? Inaonyesha ya kwamba leo hakuna woga kuhusu ukweli wa jehanamu. Hii na wahusu wanakwenda makanisani na wanaoishi kidunia. Watu hawaongopi jehanamu, ni kwa nini?

 

HITAJI LA JEHANAMU
Wanaofuuza jehanamu leo, hufanya hivyo kwa sababu kadha wa kadha. Kwanza shauku lao ni waendelee kuishi kwa dhambi, bila nafsi zao kujua matezo ya matendo yao. Hawataki kusikia wanalotenda ni makosa. Hawataki kusikia dhambi zao zitahukumiwa. Mmoja anaweza kataa. “Matezo ya milele ni jehanamu, na haiusiki na Mungu mwenye huruma na upendo. Inawezekana Mungu mwenye haki awahukumu watu kwenye jehanamu ni hitaji? Wacha tuchunguze sababu zinazozungumza kuhusu hitaji hiyo.

Utendaji wa dhambi na utakatifu wa Mungu. Uzito wa watu wengi inapokuja kuelewa na hitaji la jehanamu inahusiana na kutojua matezo ya dhambi na utukufu wa Mungu. Tunaona ubaya mkubwa ulioko kwenye dhambi ndogo au kuelewa utukufu wa Mungu, haki na gadhabu zake. Kama tungeliona dhambi kama mabaya makubwa yalioko duniani na kutambua kila dhambi kama pigamizi la maongozi ya Mungu kwetu, dharau, kofi kwa uso wake, kutupa taka kwake, tungeanza kujua kwa kifupi dhambi zetu kwake. Kila saa tunapofanya dhambi tunamwinua Mungu wa pingamizi kwenye mioyo yetu katika hali yetu wenyewe ama tunavyopenda sisi wenyewe. Dhambi ukataa Mungu muumba na kuweka sanamu badala yake

Kama tungeelewa utukufu wa Mungu na vile inamaanisha kuwa mtukufu, safi, mkamilifu, mwenye haki, kutojichafua, kusafisha hata dhambi ndogo, tungekuwa na wazo nzuri kwa nini Mungu anachukia dhambi. Utukufu mkamilifu hauwezi kuikubali hata dhambi ndogo. Habakkuk 1:13 Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye; Kama tungeweza kuelewa usafi na utukufu wa Mungu, na ubaya ulioko kwenye dhambi, basi tungekuwa na shida kuhusu hitaji lote la jehanamu.

Yeremia 17:9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? Moyo wa mwandadamu ni mgonjwa, na wenye uongo. Ufisadi wa moyo wa mwanadamu umfanya yeye kudanganywa kuhusu ubaya ulioko kwenye dhambi na mambo mengine mengi.

Mungu asiye na mwanzo wala mwisho. Kujua dhambi ni nini ni lazima tuione kupitia kwa macho ya Mungu. Mungu hana mwanzo wala mwisho na ni wa umilele. Kila tendo la dhambi ufanywa kinyume kwa Mungu mtukufu asiye na mwanzo wala mwisho. Kwa kila dhambi tunamuondoa Mungu na kujiweka juu yake. Kwa kila dhambi swala hili liko. Ni mapenzi ya Mungu au ya mwanadamu yanayofaa kutimizwa? Ya mwanadamu kwa dhambi? Mwanadamu ujiweka juu ya mapenzi ya Mungu, kwa hivyo umuweka Mungu chini ya miguu yake. Dhambi moja inayofanywa kinyume cha mapenzi ya Mungu mtakatifu asiye na mwanzo wala mwisho inafaa hukumu wa milele. Ni dhambi ya milele inayogadhabisha Mungu wa milele hata kwa mara moja.

Hukumu ya Mungu. Dhambi moja inayofanywa kwa Mungu umfanya Mungu aonyeshe jina lake na haki zake kwa kutoa hukumu. Mungu anaweza na ataonyesha haki zake. Warumi 12:19 “Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.” Ni ahadi zipi kutoka kwa mmoja wa wahubiri wakuu aliyeishi, Jonathan Edwards aliandika? Utukufu wa Mungu ni wa juu, ndiyo lengo lake la uumbaji, ni wa maana kuliko kitu kingine chochote. Lakini kuna njia vile Mungu ataonyesha utukufu wake, kwa mfano, matezo ya milele kwa wasiohaki. Watakaonyesha utukufu na haki zake. Halafu haki ipeanwe kama gavana wa ulimwengu. Haki zake Mungu ni kali, hazichelewi, zakushangaza, za kuongopya na tukufu.

 
MAELEZO KUHUSU JEHANAMU
Jehanamu ni jiko la moto usiozimika, mahali pa matezo ya milele, mahali wanao husika utezwa miili na akili zao, kulingana na makosa yao. Makosa yalioko na mwanga wa kiroho uliopeanwa kwao na kuukataa. Jehanamu ni mahali huruma na wema wa Mungu umekwisha kuondolewa, mahali gadhabu ya Mungu imefunuliwa kama moto uchomao, mahali wasiohaki uishi na mabaya yao wasioweza kuyafanya katika matezo yasiyo na mwisho.

Katika Mathayo 13:47-50 Yesu alitoa mfano kwa jaribio hilo. Kifungu 49 na 50, Bwana anaeleza kuhusu mafuno yao:Wasiohaki Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna; hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa. Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Tukiyachunguza maneno ya Bwana, kitu cha kwanza kujua ni ya kwamba Jehanamu imeelezwa kama jiko la moto. Jiko lake Nebukadinezzar (vile tunavyoelezwa kwenye angano la kale). “Jiko la kuongopya” (Danieli 3:23). Yohana mpatizaji aliongea kuhusu moto usiozimika (Luka 3:17) na ufunuo unaeleza jehanamu kama ziwa la moto (ufunuo 19:20). Tunaweza kuwaza sikitiko iliyozungumza maneno haya? Fikiria kila sehemu ya mwili ikiwekwa motoni kila mara? Kila nywele yako ikisikia matezo makubwa ya kuchomeka. Hukumu kama hii itaishi kwa muda gani? Kristo anasema kutakuwa na kilio na usaga kwa meno. Wasiohaki watalia na kusaga meno wakipitia kwenye matezo ya kuchomwa na moto kila sehemu ya mwili. Hawataweza kuokolewa.

Jonathan Edwards anaelezea kwa lugha la mrapa cemo kama miyale ya moto wa jehanamu. Wengine wenu wameshaona nyumba zikichomeka. Hakuna usaidizi kidogo kama iko katikati ya moto mkubwa. Buibui akitupwa kwa moto au mdudu mwengine ufa kwa huo moto kwa haraka sana. Hakuna kupingana na moto, hakuna nguvu za kuepuka, bali ni kutii na kujipeana kwa moto. Hii ni picha ndogo ya vile kutakuwa huko jehanamu. Bila kutubu na kumpokea Yesu Kristo jihimize wewe mwenyewe kwa vile utakuwa kana kipepeo akitupwa kwenye moto mkubwa. Jitayarishe na ujitie nguvu wewe mwenyewe tayari kupigana na miyale ya moto.

Jehanamu inaelezwa kama mahali pa ngiza. Bwana Yesu anazugumza kuhusu Mgeni aliyekuwa kwa arusi bila mavazi rasmi na akatupwa nje kwa ngiza (Mathayo 22:13). Juda anaandika kuwahusu walioko jehanamu, ambapo ngiza imeifadhiwa kwa wao milele (Yuda 13). Christopher anapenda kusema kwenye kitabu chake jehanamu ya matezo (Matezo ya jehanamu). Ngiza ni matezo na wanadamu wako tayari kuofia ngiza kuliko mwangaza. Jehanamu basi ikielezwa katika nchi kama hii ya matezo, mioyo hupatwa na hofu, kwa sababu sio ngiza tu, bali ni ngiza wa ngiza.

Jehamanu inalinganishwa na (tophet) (Isaya 30:33). “Tophet” ilikuwa mahali waaabudio Wayahudi wahabudio sanamu walitoa kafara watoto wao kwa Mungu Moloch, wakiwatupa kwenye moto. Mahali pale usiku na mchana kulisikika maombolezo na kilio, kama kilio cha usiku na mchana. Maombolezo na kilio husikika jehanamu.

Isaia anazungumza pumzi ya Bwana ni kama mto wa mawe umulikao jehanamu. Kuna ushahidi wa kutosha kwenye maandiko kuonyesya ya kwamba Mungu mwenyewe atakuwa moto wa jehanamu. Waebrania 12:28 “Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho;” Wasio haki wa dunia ucheza na kudharau kwa furaha wakati muhubiri anaongea kuhusu upendo na huruma za Mungu, lakini hawafaidiki bila ya kutubu. Kwao Mungu ni moto uchomao. Waebrania 10:30-31 “Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake. Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai.” Ni vibaya, hofu kuanguka kwa mikono ya Mungu aishie milele, hawataepuka kutoka jehanamu. Mungu atakuwa jehanamu yako na ghadhabu yake itakuteza na kukumwangikia siku zote aishiye, Zaburi 90:11 “Ni nani aujuaye uweza wa hasira yako? Na ghadhabu yako kama ipasavyo kicho chako?” kwa maana Mungu ndiye atakuwa jehanamu. Maneno hayawezi kuelezea maelezo ya jehanamu. Hakuna sababu ya kuofia hilo, pengine wachungaji wanaelezea kwa injili jambo hili zaidi ya vile ilivyo. Uwezekano huo sio vile unatakiwa bali kuna sababu ya kuamini baada ya kusema yote inawezekana, yote unayosema au kufikiria lakini ni kifuli cha ukweli.

Luka 16:19-26 Yesu anazugumzia kuhusu watu wawili. Mmoja wao alikuwa tajiri na mwingine alikuwa masikini, jina lake Lazaro. Wote wawili walikufa. Aliyekuwa masikini alibebwa na malaika mbinguni na aliyekuwa tajiri alikwenda jehanamu (Kuzimu). Tajiri hakuenda mahali pale akawe tajiri na masikini hakwenda mbinguni akawe masikini. Bwana alionyesha hadithi hii ya kufananisha hili tujue ya kwamba hali zetu ubadilika kabisa tunapopita kutoka wakati wa kuufikia umilele. Hatutakiwi kuwa wajinga na kufikiria ya kwamba kwa vile haukujaribiwa sana katika maisha haya itaendelea hivyo baada ya kifo. Maisha ya hawa wawili ya milele ilitengemea hali ya roho zao mbele za Mungu walivyokuwa wakiishi hapa duniani. Lazaro alikuwa mwaminifu kwa kumfuata Mungu. Tunaangazia hali ya tajiri kwenye andiko, kwa kuwa tuna mengi ya kujifunza kutoka kwake kuhusu jehanamu.

Mstari wa 23 na 24 zinaonyesha tajiri alikuwa kwenye matezo. Inamaanisha nini kuwa kwa matezo? Haya ni matezo ya mwili na nafsi pamoja. Kama tulivyoona mwili wa binadamu utateketezwa kwa moto mkubwa. Kila sehemu ya mwili itasikia matezo ya moto. Watu walio na maumivu makali ya tumbo husikia matezo yake, lakini uchungu ulioko jehanamu utazidi huo. Ambao wakati mwengine husababisha kifo kutokana na uchungu ulioko kwenye mwili, lakini uchungu wa jehanamu ni mwingi mno. Kama mwili wako umepitia uchungu mara kwa mara kwa wakati mmoja, haujafikia kufikia matezo ya jehanamu.

Hali zote za wanadamu zitachomeka jehanamu. Hali ya kujisikia ni hali ya kutokufa, lile andiko linazugumzia katika (Marko 9:48, Isaya 66:24) ambapo tajiri anaambiwa; kumbuka kwamba katika maisha yako watu watatezwa na uchungu mwingi kimwili, lakini wataangamizwa kwa makumbuko yake. Unakumbuka wakati uliposikia mwito na haukuitikia, ulidharau yeye). Unakumbuka wakati ulivyo onywa utubu ama ulivyo ambiwa hauwezi kupokea baraka kutoka mbinguni, kabla ya kumpokea Yesu, lakini ukadharau. Watatezwa kiwango ya kuona kama vile tajiri alivyoona utukufu wa mbingu na kujua ya kwamba wametupwa kuzimu milele. Tamaa zao hazitastaamini matezo hayo (tajiri hawezi kupata tone la maji kuweka kwenye ulimi). Watateketezwa kwa maarifa ambao hawawezi kutoroka. Watateketezwa kwa vilio, maombolezo na laana za jehanamu. Kilengo cha matezo ya manadamu hapa duniani ni kama kuumwa na mdudu ukilinganisha na matezo yaliyoko kuzimu.

Jonathan Edwards akizugumzia kuhusu hukumu ijayo ya wasio haki, inaonyesha vile hawawezi kupata nafasi ya kupumzika jehanamu. Hawakupata chochote cha kuondoa (kupunguza) matezo ya jehanamu, hakuna mahali pa pumziko pale. Hakuna mahali pa siri palio na baridi kuliko pengine, mahali wanaweza kupata pumziko kidogo. Hakuna mahali pa maji baridi katika ulimwengu huo wa matezo, hata tone la kupitia kwa mdomo. Hawana mahali pa kustarehe na kupata pumzi, hata kwa dakika, watateketezwa moto na salfa. Hakuna siku ama usiku wa kupumzika milele na milele.

 

UMILELE WA JEHANAMU
Kitu cha kushangaza kuhusu jehanamu ni wakati itaishi. Jehanamu ni ya milele na milele. Haina mwisho. Unaweza kuelewa milele? Hakuna njia yeyote ya hesabu inaweza kuelezea hilo. Akili zako haziwezi kulielewa jehanamu. Hili hali ni ya ukweli. Hali hii ya jehanamu peke yake inaweza kumfanya mwanadamu alie na kutubu. Ni ya kushangaza kwamba hali za kuepuka ukweli wa jehanamu zimeenea sana, mafundisho kama kuambiwa, kabisa (kutoishi Kwa wasio amini. Hebu tuangalie kwa mara nyingine ndio tuweze kuona ukweli wa umilele wa jehanamu ndio tuweze kuelewa jehanamu kwa njia inayofaa. Baadaye tuangalie tujue ni kwa nini ni ya milele.

Ufunuo 20:10 “Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.”Andiko hili linatuonyesha wazi muda wa jehanamu. Jehanamu ni ya milele na milele. Hakuna maelezo mengine yangetumika? Kama roho wa Mungu angependa kuzungumza na watu kwa njia ya kawaida waelewe jehanamu, ni kitu gani kingeelezea ukweli huo kuliko milele na milele. Andiko halina maelezo makubwa kuonyesha umilele, lakini milele na milele. Kwa sababu maelezo hayo yanaonyesha maisha ya Mungu mwenyewe, kuna yeyote hasijeamini Mungu ataishi milele? Ufunuo 4:9 “Na hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani, yeye aliye hai hata milele na milele,” Basi ni kwa nini shaka ubaki wakati maelezo haya yanatumika kwa zote?

Sio wazo letu kuliuliza swali hilo. Lakini kuwasaidia hili waweze kulielewa. Fikiria katikati ya moto ama jiko kubwa ambapo uchungu ni mwingi kuliko ule unaosababishwa na makaa ya moto ikikukwarusa ukiwa na joto jingi, fikiria miili yao ikiwekwa mahali kwa robo saa kama wanahisi. Ni hofu gani kuingia kwa moto huo? Na kwao inaonekana ni zaidi ya robo saa. Wakiishi kwa dakika moja hawatastaamini kufikiria kuna zingine kumi na nne zinazobaki. Je nafsi zao zitakuaje, kana unajua wanatakiwa kukaa katika haya matezo kwa masaa ishirini na nane hau mwaka mzima, hau maelfu ya miaka? Alas! Vile moyo wako ungezama kama wangejua watatezeka mwaka hadi mwaka, hakuna mwisho ama kufikia mwisho. Kufikia trilioni karne matezo yao hayatakuwa karibu na mwisho kuliko mwanzo, na hakuna kuwachiliwa, lakini matezo ya jehanamu yatakuwa makubwa kuliko vile inavyofikiriwa.

Bwana Yesu Kristo akielezea siku ya hukumu ya mwisho, inaonyesha kutenganishwa kwa wenye haki na wasio haki Mathayo 25:46 “Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.” Kuna yeyote anayekana mbingu inaishi milele na milele? Je kuna muongozo siku zijazo unaoweza kutoa baraka za mbingu? Kwa hakika hapana, ijapokuwa neno hilo la ugiriki inayotumika kwenye andiko kuelezea uzima wa milele kwa wenye haki ndilo linalotumika kwa hukumu ya milele kwa wasio haki. Jehanamu litaishi kama mbingu litaishi.

Jehanamu kutakuwa na viwango tofauti vya hukumu kutolewa kwa kila mtu kulingana na andiko hili Luka 12:47-48

Alujua mapenzi ya babaye, na hakujitayarisha mwenyewe hau kutenda kulingana na mapenzi yake, kupigwa na mijeredi, na Yule hakutenda kitu chochote kingefaa mijeredi, atapigwa na michache. Na kwa Yule ameaminiwa kwa mingi, mingi ataitishwa Yesu anasema. Andiko ilioko kwenye “Mathayo11:24 Klisto anasema ya kwamba Mathayo 11:24 “Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe.” watu wa Capernaumi watapewa hukumu kubwa kuliko wale waliishi Sodoma. Luka anaelezea kiwango cha hukumu kulingana na mwanga uliopokelewa. Wengine watapata kidogo na wengine watapata nyingi.

Wale wanapotenda dhambi kubwa watahadhibiwa kiwango cha juu zaidi kuliko wale wliotenda dhambi ndogo huko jehanamu. (yohana 19:11). Wanafiki wa kidini wanaojiita Wakristo watapata hukumu kubwa kuliko wengine wowote (Mathayo 23:14-15). Yesu aliongea kuhusu Juda Iskarioti. Mathayo 26:24 “Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.” Ungewezaje kuyaona makosa kama ingekuwa kweli kuaribiwa huko hata baada ya kufa? Kuweko kwa viwango tofauti vya hukumu ya jehanamu itasikika kwa utofauti, ingewezekana aje kusemwa kwa juda iskariote ni afadhali kama haungezaliwa kama kuaribiwa kabisa ndivyo ulikuwa unatarajia? Kuaribiwa kabisa ama kusimamishwa kuishi siyo hukumu kabisa.

Kila wakati asiye haki utenda dhambi uongeza kiwango cha hukumu yake jehanamu. Anayefanya dhambi mara mbili kwa mwanga mmoja atapata viwango viwili kwa dhambi hiyo. Kila wakati mwenye dhambi anaendelea kuishi hapa duniani bila kutubu uongezea hukumu yake jehanamu. Warumi 2:5 “Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,” Bwana Yesu Kristo aliwaimiza wenye haki kuweka hazina zao mbinguni kuliko hapa duniani. Wasio haki uongezea gadhabu na hukumu jehanamu kila siku wanapotenda dhambi. Wanaongezea hukumu yao kila siku. Jehanamu watu watajuta hawangezaliwa.

Charles HaddonSpurgeon alisema, hakuna tumaini lolote hata ya kufa. Tumaini ya kuokolewa imepotea kabisa kwenye pigu za jehanamu. Imeandkwa milele kwenye moto wa jehanamu maneno haya yameangaziwa. Juu ya vichwa vyao wanaweza kuyasoma maneno haya milele. Vitendo vyake havijahusishwa na wazo la moyo inauma milele. Alas, kama ningewaambia leo jioni jehanamu izimwe siku moja wanaopotea waweze kuokolewa, kungekuwa na sherehe kubwa jehanamu lakini hiyo haiwezekani. Ni milele kwa waliotupwa nje kwa giza.

Christopher Love anatoa mfano hili tuweze kuelewa umilele. Fikiria kama milima yote ya dunia ingekuwa milima ya changarawe, na milima nyingine kuongezwa iweze kufikia mbingu, na ndege achukue mbegu moja ya changarawe kwa miaka elfu moja kutoka kwa huo mlima mkubwa, basi kungechukua miaka mamillion haiwezi kuhesabika kabla ya mlima huyo kuisha, na mwisho mlima huo utakuja kuisha, na ingekuwa furaha kwa mwanadamu kama jehanamu haingeweza kuishi zaidi ya hiyo. Lakini matezo ya mwanadamu jehanamu hatakuwa na nafasi ya kutoka baada ya kuchukua mamilioni ya miaka tangu alipotupwa hapo, kwa maana matezo haya ni ya milele, haina mwisho, kwa sababu Mungu anayewahukumu ni wa milele.

Hapo awali tumeona umuhimu wa jehanamu kuwa mahali kama hapo. Tunazungumza ni kwa nini jehanamu siyo iwe, bali ni ya milele. Ni kwa nini jehanamu ni ya milele? Kuna majibu kadha wa kadha tunaweza kuyaangalia kwa ufupi.

Sababu ya kwanza tunaweza kufikiria ni hile Christopher Love ametaja. Mungu anayelaani ni wa milele. Umilele wa jehanamu ni kutokana na maisha ya Mungu. Ni neno ya umilele wa Mungu. Waebrania 13:8 Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele. Zaburi 111:3 Kazi yake ni heshima na adhama, Na haki yake yakaa milele I Petro 1:24 Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka. Kama haki za Mungu ni za milele na Mungu ni wa milele, basi ni kwa nini hawezi kuwa na gadhabu ya milele? Kwa vile Mungu anaishi milele basi heshima zake ni za milele na hazibadilishwa milele basi heshima zake ni za milele na hazibadiliki. Kwa hivyo, jehanamu inavyoelezewa na gadhabu ya Mungu lazima iwe ni ya milele.

Jehanamu lazima iwe ni ya milele, kwa sababu haki za Mungu hazitatimizwa na watenda dhambi wasio na mwisho, haijalishi ni muda gani. Yesu anafafanua hayo anavyosema weka amani ya adui yako kabla ya kwenda kwa hakimu usije ukatumwa jela. Luka 12:59 “Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.” Mwanadamu hana kitu cha kupeana kwa makosa yake. Hakuna kipimo cha hukumu, hata kama umeishi hapo mda gani hili iwe kama msamaha wa dhambi. Haiwezekani, kwa hivyo jehanamu ni ya milele.

Ya tatu jehanamu ni lazima iwe ni ya milele, kwa sababu maandiko yanasema mdudu anayekula mwanadamu jehanamu hatakufa. Isaya 66:24 “Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.” Kama mdudu hatakufa basi wale wanateketezwa jehanamu hawatakufa.

Ya mwisho, jehanamu ni ya milele kwa maana watu wanazidi kutenda dhambi huko. Wanaendelea kuongezea na kukusanya makosa yao huko. Jehanamu ni mahali waliotupwa huko umlahani Mungu na wao wenyewe. Na wanakanusha na lugha za wanafiki za watu. Matezo ya wasio haki yanaongezeka kwa kuwalahumu na kuwalaani wenzao. Wanadamu hawatatubu jehanamu kwa maana tabia zao hazitabadilika. Wangali wenye dhambi. Watatenda dhambi milele, kwa hivyo Mungu atawahukumu milele.

 

MAOMBI KWA WANAO AMINI NA WASIO AMINI
Angano la kale inazidi kutustaajabisha na matezo ya jehanamu: Isaya 33:14 Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto ulao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele? Nahum 1:6 Ni nani awezaye kusimama mbele za ghadhabu yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira yake? Hasira yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na yeye. Wenye dhambi, unadhani utaweza kustaamini gadhabu ya Mungu inapo kunyeshea kwa kiwango kikubwa kama hicho? Unaweza kufikiria jehanamu siyo moto vile unavyo inuka na kutazama. Kama unaamini hivyo huko zaidi ya mjinga. Matezo ya jehanamu ufanya hata mapepo kutetemeka.Ungali mjinga kwa kubakia kwa hiyo na kuyachukua kwa urahisi?