Jesus as Personal Savior

Je, inamaanisha nini kumkubali Yesu kama mwokozi wako?

Je, umeshawahi kumkubali Yesu kama mwokozi wako? kabla hujajibu, niruhusu nikueleze swali hili. Ili kwakuweza kulielewa swali hili vizuri, ni sharti mwanzo umwelewe vizuri “Yesu Kristo,’’ “Kibinafsi” na “Mwokozi.’’

Yesu Kristo ni nani? Watu wengi humtambua Yesu Kristo kama mtu mzuri, Mwalimu Mkuu, au hata pia Nabii wa Mungu. Haya maelezo huenda yakawa ni kweli kabisa kuhusu Yesu, lakini hayaelezei vizuri yeye ni nani. Bibilia inatuambia yakwamba Yesu ni Mungu katika mwili, Mungu alifanyika kuwa mwanadamu (Tazama Yohana 1:1, 14). Mungu alikuja ulimwenguni kutufundisha, kutuponya, kuturekebisha, kutusamehe-na kufa kwa ajili yetu! Yesu Kristo ni Mungu, Muumbaji, Mungu Mkuu. Je umemkubali huyu Yesu?

Je, Mkombozi ni nini na kwanini tunahitaji Mkombozi? Bibilia inatwambia yakwamba sote tumefanya dhambi, sote tumetenda maovu (Warumi 3:10-18). Kwa wajibu wa dhambi zetu, basi twastahili hasira za Mungu na pia hukumu. Adhabu ya pekee kwa kufanya dhambi kinyume chake asiye kuwa na mwisho na Mungu wa milele ni adhabu isiyokuwa na mwisho au mipaka (Warumi 6:23; Ufunuo wa Yohana 20:11-15). Hii ndio sababu tunahitaji Mkombozi!

Yesu Kristo, alikuja duniani na akatufia pahali petu. Kifo chake Yesu, kama Mungu katika mwili, ilikuwa ni malipo yasiyokuwa na mwisho kwa ajili ya dhambi zetu (2 Wakorintho 5:21). Yesu alikufa ili kutulipia mshahara wa dhambi zetu (Warumi 5:8). Yesu alitulipia deni ili tukaweze kuwa na uhuru. Kufufuka kwake Yesu katika wafu kulidhihirisha yakwamba kifo chake kilitosha kulipa mshahara wa dhambi zetu. Hii ndiyo sababu yakuwa Yesu Kristo ndiye Mkombozi tu wa pekee (Yohana14:6; Matendo 4:12)! Je, unamwamini Yesu kama mwokozi wako?

Je, Yesu ni Mwokozi wako “Wa Kibinafsi’’? Watu wengi huchukulia yakwamba ukristo ni kuhudhuria kanisa, Kutoa makafara, kutofanya dhambi Fulani. Hiyo siyo Ukristo. Ukristo wa kweli ni ule uhusiano wa kibinafsi na Yesu Kristo. Kumkubali Yesu kibinafsi kama mwokozi wako inamaanisha kuweka imani yako kibinafsi kwake na kumwamini yeye. Hakuna aokokaye kupitia imani ya wengine. Hakuna asamehewaye kwa kutenda matendo aina Fulani. Njia ya pekee ya wokovu ni kumkubali Yesu kibinafsi kama mwokozi wa maisha yako, kuamini kifo chake kama malipo ya dhambi zako, na kufufuka kwake kama hakikisho kwako la uzima wa milele (Yohana3:16). Je, Yesu kibinafsi ni Mwokozi wako?

Kama ungetaka kumkubali Yesu Kristo kibinafsi kama Mwokozi wako, Hebu yaseme maneno haya kwa Mungu. Kumbuka kwa kuomba ombi hili au ombi lengine lolote lile haitaweza kukuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo pekee ndiko kuwezako kukuokoa toka dhambini. Ombi hili ni kwa kumwelezea Mungu imani yako kwake na kwa kumshukuru kwa kukupea wokovu.

“Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo aliichukua adhabu niliyostahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ninamkubali Yesu kibinafsi kama Mwokozi wangu! Ahsante kwa neema yako ya ajabu na kwa msamaha-karama ya uzima wa milele! Amina!’’




AMAZING GRACE BIBLE INSTITUTE