Je, Yesu ndiye njia ya pekee ya Mbinguni?Mimi ni mtu mzuri, kwahivyo nitaenda Mbinguni. “Sawa, kwahivyo nafanya mambo mabaya, lakini zaidi nafanya mambo mazuri, kwahivyo nitaenda Mbinguni.” Mungu hatanipeleka Jehanamu kwasababu siishi kulingana na Bibilia. Nyakati zimebadilika!’’ “Watu wabaya pekee kama vile watesaji watoto na wauaji huenda Jehanamu.” Haya yote ni mafikira ya kawaida kati ya wengi, lakini ukweli ni kwamba yote ni uongo. Shetani mtawala wa dunia, huyapanda mafikira/mawazo haya akilini mwetu. Yeye na yeyote afuataye njia zake ni adui wa Mungu (1Petro 5:8). Shetani hujigeuza na kujifanya mzuri (2Wakorintho 11:14), lakini anauwezo juu ya akili zote ambazo hazimwelekei Mungu. “Shetani, Mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake. Hawaielewi injili kuhusu utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu” (2Wakorintho 4:4). Ni uongo kuamini ya kwamba Mungu hashuhuliki na dhambi ndogo, na kwahivyo Jehanamu imetengewa “Watu wabaya.” Dhambi zote zinatutenganisha na Mungu, hata “ile dhambi ndogo nyeupe.” Wote wamefanya dhambi, na hakuna atoshaye kuwa mzuri wa kujifikisha Mbinguni yeye mwenyewe (Warumi 3:23). Kuingia Mbinguni haitegemei kwamba uzuri wetu uwe unazidi ubaya wetu, Sote tungelishindwa kama hiyo ndiyo hali. Na ikiwa wanaokolewa kwa neema yake Mungu, basi sio kwa matendo yao mazuri. Kwasababu hiyo, neema yake Mungu isingekuwa kama jinsi ilivyo-ya huru na isiyostahili (Warumi 11:6). Hatuwezi kufanya lolote jema lakutuwezesha kufika Mbiguni (Tito 3:5). Unaweza kuingia katika ufalme wa Mungu kwakupitia mlango ulio mwembamba pekee. Njia ya Jehanamu ni pana na mlango wake ni mpana kwa walio wengi wachaguao njia ya rahisi (Mathayo 3:13). Hata kama kila mtu anaishi maisha ya dhambi, na kumwamini Mungu hakumo, Mungu hatasema hivyo. “Ulikuwa ukiishi kama kawaida ya ulimwengu huu, uliojaa dhambi, ukimtii Shetani mfalme wa uwezo wa anga. Yeye ni roho atendaye kazi katika mioyo ya wale wakataao kumtii Mungu” (Waefeso 2:2). Wakati Mungu alipoumba ulimwengu, ulikuwa kamili. Kila kitu kilikuwa kizuri. Halafu akamuumba Adamu na Hawa na akawapa uhuru ili waweze kuwa na chaguo kama watamfuata na kumtii Mungu au la. Lakini Adamu na Hawa, wanadamu wa kwanza kabisa Mungu alioumba walidanganywa na Shetani wamuasi Mungu, na wakatenda dhambi. Hii iliwatenganisha (na kila aliyekuja baada yao pamoja na sisi) na uwezo wakuwa na uhusiano wakaribu na Mungu. Yeye ni mkamilifu na hawezi kuwa penye dhambi. Kama watu wenye dhambi, hatungeliweza kufika huko sisi wenyewe kwahivyo, Mungu akatengeza njia ili tuweze kupatanishwa naye huko mbinguni. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu’’ (Warumi 6:23). Yesu alizaliwa ili aweze kutufundisha / kutuonyesha njia na afe kwa ajili ya dhambi zetu. Siku tatu baada ya kifo chake, alifufuka toka kaburini (Warumi 4:25), akishuhudia ushindi wake juu ya mauti. Aliliunganisha pengo kati ya Mungu na mwanadamu ili tukaweze kuwa na uhusiano wa kibinafsi naye kama tutaamini. “Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yohana17:3). Watu wengi wamwamini Mungu, hata Shetani pia. Lakini kupokea wokovu, ni sharti tumregelee Mungu, tujenge uhusiano wa kibinafsi, tuziache dhambi zetu na tumfuate yeye. Ni sharti tumwamini Yesu kwa kila kitu tulicho nacho na kwakila tunachofanya. “Tunafanywa kuwa wenye haki mbele za Mungu tunapomwamini Yesu Kristo atuchukulie dhambi zetu. Na sote tunaweza kuokolewa namna hii, haijalishi sisi ni kina nani au tumefanya nini’” (Warumi3:22). Bibilia inafundisha yakuwa hakuna njia nyengine yoyote ya wokovu isipokuwa kupitia kwa Kristo. Yesu asema katika Yohana 14:6, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima, mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Yesu ndiye njia ya pekee ya wokovu kwasababu yeye pekee anaweza kutulipia adhabu ya dhambi zetu (Warumi 6:23). Hakuna dini nyengine yoyote ifundishayo kwa kina au uzito wa dhambi na madhara yake. Hakuna dini nyengine yoyote inayogarimia malipo ya dhambi isipokuwa Yesu pekee. Hakuna “mwanzilishi wa dini” mwengine ambapo Mungu alifanyika kuwa mwanadamu (Yohana1:1, 14) - njia ya pekee ya kuweza kulipa deni. Ilibidi Yesu kuwa Mungu ili aweze kutulipia deni. Ilibidi Yesu afanyike kuwa mwanadamu ili aweze kufa. Wokuvu unapatikana kwa imani ndani ya Yesu Kristo! “Wala hakuna wokovu katika mwengine |