Ninawezaje kuwa mwana wa Mungu.“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12). Lazima uzaliwe mara ya piliWakati alitembelewa na kiongozi wa dini, Nikodemo, Yesu hakumwakikishia mbunguni papo hapo. Badala, Kristo alisema, “Amini, amini, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu” (Yohana3:3). wakati mtu anapozaliwa mara ya kwanza, anarithi ile hali ya dhambi ambayo yatokana na kutotii kwa Adamu katika bustani mwa Edeni. Motto haitaji kufunzwa na mtu yeyote kutenda dhambi. Kimaumbile anaifuata ile tamaa ya dhambi, nayo inamwelekeza kudanganya, kuiba, na kuchukia. Badala ya kuwa mwana wa Mungu, ni mototo wa kutotii na wa ghadhabu. “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika tama za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili nay a nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine” (Waefeso 2:1-3). Kama watoto wa ghadhabu, tunastahili kutenganishwa na Mungu jahannam. Shukrani kubwa kwa Mungu kwa sababu ya ujumbe ufuatao ambao wasema, “Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yatu;alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema” (Waefeso 2:4-5). Je! Tumefanywa hai pamoja na Kristo/kuzaliwa mara ya pili/kufanyika wana wa Mungu namna gani? Lazima tumpokee Yesu! Mpokee Yesu“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12). Ufahamu huu wazi waeleza jinzi ya kufanyika mwana wa Mungu. Lazima tumpokee Yesu kwa kumwamini. Tunastahili kuamini nini juu ya Yesu? Kwanza, lazima tutambue kwamba Yesu ni mwana wa Mungu milele ambaye alikuwa mwanadamu. Alizaliwa kupitia kwa nguvu za Roho Mtakatifu na bikra Mariamu, Yesu hakurithi hali ya dhambi kutoka kwa Adamu. Kwa hivyo, anaitwa Adamu wa pili (1Wakorintho 15:22). Huku kwa kutotiii kwa Adamu kulileta laana ya dhambi ulimwengu, maishia makamilifu ya Yesu yanaweza kufunika yale ya dhambi. Itikio letu lazima liwe la kutubu (igeuke dhambi), kwamini maisha Yake makamilifu yatutakaze. Pili, lazima tuwe na imani kwa Yesu kama mwokozi. Mpango wa Mungu ulikuwa kusulubisha mwanawe mkamilifu msalabani kulipa adhabu tuliyohistahili kwa ajili ya dhambi zetu: kifo. Kifo cha Yesu kinawaweka huru wale wote wanaompokea kutoka kwa nguvu ya dhambi. Mwisho, latumfuate Yeso kama Bwana. Baada ya kumfufua Yesu kama mshindi wa dhambi na mauti, Mungu alimpa mamlaka yote (Waefeso 1:20-23). Yesu anawaongoza wale wote wanaompokea; na atawahukumu wale wote wanaomkataa (Matendo Ya Mitume 10:42). Kwa nehema ya Mungu ambayo inatusaidia kutubu na kuwa na imani katika Mwokozi na Bwana, tumezaliwa maisha mapya kama wana wa Mungu. Ni kwa wale pekee watakao mpokea Yesu- sio kujua tu kuhusu Yeye pekee bali kumtegemea kwa wokovu, kunyenyekea kwake kama mkuu wetu, na kumpenda kama dhamani yetu kuu- itakufanya kuwa mwana wa Mungu. Fanyika mwana wa Mungu“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu” (Yohana 1:12-13) Kama vile hatukuchangia kitu chochote kwa kuzaliwa kwetu kwa mwili wa kawaida, vile vile hatuwezi kuwa katika jamii ya Mungu kwa nguvu zetu au kwa matendo yetu mazuri au kufanyia imani yetu mazingaombwe. Vile aya hapo juu zinasema, Mungu ndiye “aliwapa uwezo” kulingana na mapenzi yake ya nehema. “Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu” (1Yohana 3:1). Kwa hivyo mwana wa Mungu hana kitu cha kujivunia, bali kuvunia kuwa ndani ya Yesu (Waefeso 2:8-9). Mto hukua ili awe kama wazazi wake. Vile vile, Mungu anataka watoto wake zaidi na zaidi kama Yesu Kristo. Ingawa ni mbinguni pekee tutakuwa wakamilifu, mwana wa Mungu hawezi kuwa na mazoea, ya kuendelea kutenda dhambi bila kutubu. “Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, walaa yeye asiyempenda ndugu yake” (1 Yohana 3:7-10). Usifanye makosa; mtoto wa Mungu hawezi “kanwa” kwa kutenda dhambi. Lakini kwa Yule anayeendelea kutenda dhambi (kwa mfano, anaendelea kufurahia dhambi bila kusikia maagizo ya kumfuata Kristo na Neno lake) yaonyesha kwamba hakuwai zaliwa mara ya pili. Yesu alisema kuhusu watu kama hao, “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tama za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda” (Yohana 8:44). Watoto wa Mungu, kwa upande mwingine, hawatamani tama za dhambi bali watamani kujua, upendo na utukufu wa Baba yao. Taji ya kuwa mtoto wa Mungu haipimiki. Kama mtoto wa Mungu, sisi tuko sehemu ya jamii yake (kanisa), tumeaidiwa makao mbinguni, na kupewa uwezo wa kumsongea Mungu katika maombi kama Baba (Waefeso 2:19; 1Petero 1:3-6; Warumi 8:15). |