Ninawezaje kuokoa?
Hii ni rahisi, lakini ni swali la muimu ambalo linaweza kuulizwa. “Ninawezaje kuokoka?”, linaangazia ni wapi tutaishi milele baada ya maisha yetu humu duniani yameisha. Hakuna kitu muhimu kuliko hatima yetu ya milele. Shukrani kwa Biblia ii peupe jinsi mtu anaweza okoka. Mfungwa wa Filipi alimuuliza Paulo na Sila, nitafanya nini ili niokoke?” (Matendo Ya Mitume 16:30). Paulo na Sila wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu, na utaokoka (Matendo 16:31).
Ninawezaje kuokoa? Ni kwa nini ninahitaji kuokoka?
Wote tumeadhirika na dhambi (Warumi 3:23). Tunazaliwa na dhambi (Zaburi 51:5), na sisi wote tulichagua kutenda dhambi (Mhubiri 7:20; 1Yohana 1:8). Dhambi ndio kitu kinatufanya tusiokoke. Dhambi ndio ututenganisha na Mungu. Dhambi ndio imetuweka katika barabara iendeayo kuzimuni.
Ninawezaje kuokoa? Kuokolewa kutoka kwa nini?
Kwa sababu ya dhambi zetu sisi wote tunastahili kifo (Warumi 6:23). Huku ikiwa mshahara wa dhambi ni mauti, hicho sio kifo pekee kinatokana na dhambi. Dhambi zote zinatendwa kinyume na Mungu aishiye milele (Zaburi 51:4). Kwa sababu ya hiyo, adhabu ya haki ya dhambi zetu ni ya milele. Chenye tunastahili kuokolewa kwalo ni ule uharibifu wa milele (Mathayo 25:46; Ufunuo 20:15).
Ninawezaje kuokolewa? Ni namna gani Mungu ameutoa wokovu?
Kwa sababu adhabu ya haki ya dhambi ni ya milele, ni Mungu pekee ataweza kuilipa, kwa sababu yeye ni wa milele. Lakini Mungu kwa uungu wake hawezi kufa. Kwa hivyo alifanyika mwanadamu katika Kristo Yesu. Mungu aliuchukua mwili wa mwanadamu, akaishi nasi, na akatufunza. Wakati watu walimkataa na ujumbe wake, na wakatafuta kumwua, kwa kupenda kwa akajitolea kusulubiwa kwa ajili yetu (Yohana 10:15). Kwa sababu Yesu Kristo alikuwa mwanadamu, angekufa, kwa sababu Yesu Kristo alikuwa Mungu, kifo chake kilikuwa cha dhamani ya milele. Kifo cha Yesu msalabani ndio fidia kamilifu ya dhambi zetu (1Yohana 2:2). Alichukua adhabu ambayo tulistahili. Kufufuka kwa Yesu utoka kwa wafu kwaonyesha kuwa kifo chake hakika kilikuwa dhabihu kamili ya dhambi zetu.
Je! Ninawezaje kuokoka? Ninastahili kufanya nini?
“Amini katika Bwana Yesu na utaokolewa” (Matendo 16:31). Mungu amekwisha fanya kazi yote. Chenye unastahili kufanya ni kupokea kwa imani wokovu ambao Mungu anautoa (Waefeso 2:8-9). Kamilifu mwamini Yesu pekee kama dhabihu ya dhambi zako. Mwamini yeye na hautaangamia (Yohana 3:16). Mungu anakupa wokovu kama tuzo. Chenye unastahili kufanya ni kuikubali. Yesu ndiye njia ya wokovu (Yohana 14:6).
|