TAZAMA MWANA KONDOO WA MUNGU




“Kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka wafu, utaokoka. Maana tunaamini kwa moyo na kukubaliwa kuwa waadilifu; na tunakiri kwa midomo yetu na kuokolewa. Maana Maandiko Matakatifu yasema: "Kila mtu atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa."
Warumi 10:9,10,13


Kwa hivyo, ufufuo wa wafu una maana gani na wokovu wetu?





Kufukuka kwa Kristo – Kumeanzisha umuhimu wake

Mtume Paulo ameweka wazi katika waraka wake kwa Wakorintho: "Kama hakuna ufufuo wa wafu, basi, Kristo naye hakufufuka;:" 1 Warorintho 15:13. Katika sura hiyo pia anasema “tena kama Kristo hakufufuka, basi,kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure; mngali kwa dhambi zenu 1wakorintho 15:14.

Umuhimu wa kufufuka kwa Kristo umeonyeshwa kwa jinsi vile umetiliwa mkazo na kuhuburiwa na kanisa la kwanza.(kwa mfano, Matendo ya Mitume 2:31; 4:33; 17:18; 26:23). Karibu kila yeyote shahidi wa injili akieleza kuhusu ufufuo wa Kristo, anatilia mkazo ya kwamba huo ndio tumaini ya wale wanao okoka.

Maandiko yasema hivi, “Mimi niliwakabidhi ninyi mambo muhimu sana ambayo mimi niliyapokea: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na Maandiko Matakatifu; kwamba alizikwa, akafufuka siku ya tatu kama ilivyoandikwa;” 1 Wakorintho 15:3-4.

Cha muhimu kabisa, Biblia inasema sababu ya kifo na kufufuka kwa Yesu kama ndio pekee inayofungua njia ya mbinguni.


Maana mshaara wa dhambi ni mauti.

Mungu aliumba nchi na binadamu kamilifu. Lakini wakati Adamu na Eva walikataa kutii maangizo ya Mungu, Mungu aliwaadhibu. Akimu anayewasamehe wenye – kutotii sheria yeye sio akimu wa haki. Hivyo ndivyo ilivyo, kutojali dhambi kuweza kumuweka Mungu mtakatifu aonekane kama asiyekuwa wa haki. Kifo ndicho adhabu ya haki iliyomstahili Mungu kupeana kwa sababu ya dhambi. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” (Warumi 6:23).

Hata sio kwa matendo mazuri yetu, yanaweza kulipia mabaya yetu. Kulinganisha na uzuri wake, “na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi” (Isaya 64:6b). Tangu dhambi ya Adam, kila binadamu amekuea mwenye dhambi kwa kutokutii sheria za Mungu. “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” (Warumi 3:23) Dhambi sio hatini mambo makubwa kama kuua, ama kutusi, mbali inahusisha tamaa ya fedha, kuchukia maadui, ulimi wa uongo na kiburi, kwa sababu ya dhambi, kila mtu alistahili kifo – kutengana na Mungu kwa milele na milele jehanamu.


Ahadi iliyo stahili kifo cha aliye mtakatifu.


Tazama mwana kondoo

Ingawa Mungu aliwafukuza Adamu na Eva kutoka kwa shamba, Hakuwaacha bila matumaini ya Mbingu. Aliwaaidi atatuma dhabiu isiyokuwana dhambi kuondoa adhabu iliyowastahili. (Mwanzo 3:15)..Hapa ndipo pana mpango kamilifu wa Mungu: Mungu mwenyewe alitoa sadaka (Yesu) yule angekuwa upatanisho wa dhambi. Mwana mtakatifu wa Mungu, alitimiza matakwa ya ukamilifu wa sheria takatifu za Mungu. “Kwa yeye (Mungu) alimfanya huyo (Kristo) kuwa dhambi kwa sisi, yule (Yesu)hakujua dhambi yeyote; hili tuweze kufanywa watakatifu wa Mungu ndani yake (Yesu)”. 2 Wakorintho 5:21

Yesu alikufa msalabani, akawekwa kaburini kudhibitisha kifo chake, kwa kwa ushindi akafufuka siku ya tatu baadaye.

Kifo cha Yesu kilikuwa na maana kama vile tu dhambiu yake ya damu. Na maana sawasawa kuwekwa kaburini na kufufuka kwake; LAKINI kingine chochote kuyahusu maisha ya Yesu kulionyesha damu yake inayo zungumziwa mbinguni. " Webrania 9:24-26 yasema, Maana Kristo hakuingia Mahali Patakatifu palipojengwa kwa mikono ya watu, ambapo ni mfano tu wa kile kilicho halisi. yeye aliingia mbinguni kwenyewe ambako sasa anasimama mbele ya Mungu kwa ajili yetu. Kuhani Mkuu wa Wayahudi huingia Mahali Patakatifu kila mwaka akiwa amechukua damu ya mnyama; lakini Kristo hakuingia humo ili ajitoe mwenyewe mara nyingi, maana ingalikuwa hivyo, Kristo angalipaswa kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa ulimwengu. Lakini sasa nyakati hizi zinapokaribia mwisho wake, yeye ametokea mara moja tu, kuondoa dhambi kwa kujitoa yeye mwenyewe dhabihu.

"Yeye aliingia Mahali Patakatifu mara moja tu, tena hakuwa amechukua damu ya mbuzi wala ng'ombe, bali aliingia kwa damu yake yeye mwenyewe, akatupatia ukombozi wa milele. - Webrania 9:12



Yesu, mwana kondoo mtaktifu wa Mungu alisulubiwa msalabani sio kwa sababu kuna mabaya alitenda, lakini kwa sababu ya upendo wake kwako na mapenzi yake ukaishi naye mbinguni milele.



Tumwelekee Yesu ambaye ndiye aliyeianzisha imani yetu na ambaye ataikamilisha. Kwa ajili ya furaha iliyokuwa inamngojea, yeye alivumilia kifo msalabani, bila kujali juu ya aibu yake, na sasa anaketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.

Waebrania 12:2

Tazama kwa kuonyesha nguvu za Mungu, kufufuka kwa Yesu kumetosha kulipia deni ya kifo na utengano uliokuwa katikati yetu na Mungu – kwa sheria. Dhambi moja kutokulipiwa, kungalimaanisha bado kuna adhabu ya kifo na Yesu yu angali kaburini. Na kama kuna dhambi moja kuhesabiwa katika nafsi yako. Basi ingalimaanisha Yesu asulubiwe tena. “iyo ni haiwezekani” Biblia yasema. Webrania 6:4 Maana watu wanaoiasi imani yao inawezekanaje kuwarudisha watubu tena? Watu hao walikwisha kuwa katika mwanga wa Mungu, walikwisha onja zawadi ya mbinguni na kushirikishwa Roho Mtakatifu;."


“nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu,
lisiwapate pigo lolote likawaharibu,”
Kutoka 12:13



Tumeokolewa: kutoka kwa adhabu ya dhambi (Waefeso 2:8, 9). Huu ndio unaitwa wokovu wa kuhesabiwa haki.

Tunaokolewa; kutoka kwa nguvu za dhambi, anayetenda haya; ni Roho Mtakatifu, wakati kwa wakati (Warumi 6). Hii ndio inaitwa kutakaswa.

Tutaokolewa: kuondolewa mbele za dhambi; baada ya ufufuo, hii ndio inaitwa kutukuza, ama “ukombozi wa mwili wetu” (Warumi 8:23).






Msingi wa ulinzi wetu:

Tume kombolewa na damu ya Yesu



Nguvu za MUNGU

Inategemea na Mungu Baba:

1) Bali kwa kadiri ya makusudi yake

Kusudi yake ya milele hapa iko (Waefeso 1:11-12). Kusudu hili la milele imefichwa kwa pazia na kudhibitishwa na kiapo (Waebrania 6:17-20). Tena imefananishwa na mambo matano yasiyovunjika katika kitabu cha Warumi 8:

"Tunajua kwamba, katika mambo yote, Mungu hufanya kazi na kuifanikisha pamoja na wote wampendao, yaani wale aliowaita kufuatana na kusudi lake. Maana hao aliowachagua tangu mwanzo, ndio aliowateua wapate kufanana na Mwanae, ili Mwana awe wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Basi, Mungu aliwaita wale aliokuwa amewateua; na hao aliowaita aliwakubali kuwa waadilifu; na hao aliowakubali kuwa waadilifu aliwashirikisha pia utukufu wake." - “ Warumi 8:28-30

2) Juu ya ahadi yake ya kweli

Wokovu wetu utengemea ahadi zake, Bali sio bidii yetu kwa vyovyote:
Kwa hivyo ni kwa imani [hakuna kazi ya mtu hapa] ili iweze kuwa ni kwa neema [mambo yote hapa ni kazi ya Mungu]; ili mpaka mwisho ahadi yake iwe ya kweli... Warumi 4:16
Kama inategemea kwa vyovyote uwezo wa binadamu kuendelea kuamini , basi ahadi haiwezi kubaki imara. Ahadi za wale wanaoamini wokovu zimedhibitishwa kila mahali (Mwanzo 15:6; Yoana 3:16: Matendo ya Mitume 16:33; Warumi 4:23-24, na kuendelea)

3) Juu ya nguvu zake zisizo na kipimo

Yeye yuko huru kutuokoa. Kifo cha Kristo kimemfanya Mungu kwa bure kutuokoa sisi ingawa hatufai. Ulinzi wetu wa milele hautengemei uzuri wetu. Yesu ndiye mpatanishi kwa dhambi zetu (1 Yohana 2:2) kudhani ya kwamba kuna dhambi zingine ambazo zinazoweza kufanya tupoteze wokovu wetu hiyo ni kudhani ya kwamba atufahi wokovu baada ya kutenda hii dhambi kuliko vile tuliitenda hapo awali. Na kuamini hivyo-kunapunguza wokovu chini kwa uwezo wa binadamu). Yeye amekusudia kutudumisha kwa wokovu: na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho. Yohana 6:39 na: Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hauka mtu anakayewapokonya katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. Yohana 10:28-29 “Kamwe: katika Yohana 28 ni kinyume mara mbili,

4) Juu ya “wingi wake” wa upendo

Kusudi lake limejengwa juu ya upendo (Warumi 5:6-10): Mungu alijua wakati alituokoa ya kwamba tulikuwa tumepotea kwa dhambi, na kwa hivyo jambo jipya la dhambi kwa maisha yetu baada ya wokovu haliwezi kwa vyovyote kumfanya Mungu angeuze mawzo yake aondolee mbali rehema na wokovu wake kwetu. (Warumi 11:29; Warumi 8:32, 38-39).

Alituoka sisi kwa sababu sizizo zetu lakini zake kando na sisi. Ilikuwa ni kwa anjili ya kutiwa moyo na upendo wake, lakini sio kwa kuangalia yale mazuri ya mwenye dhambi.

5) Juu ya majibu ya maombi ya Mwanawe

Sisi, kama walioamini, tunayo majina tofauti kwa Bibilia: watakatifu, walioamini, wateule, kondoo, waridhi, lakini jina lililo la muhimu mkubwa ndani ya Kristo limerudiwa mara saba kwa maombi yake ya kuani mkuu (Yoahana 17): “Hao ulionipa” (Yohana 17:11-12). Yesu anaomba kwamba tusiende Jahanamu (Yohana 17:15) na tutakuwa pamjoa naye mbinguni (Yohana 17:20,24). [Kutakaswa huku ni kwa anjili tusipotee, lakini si kuridhi kila kitu] naamini ya kwamba Mungu baba wakati wote anajibu maombi ya mwanawe (Yohana 11:42).


Upendo wa Yesu

Inausu juu ya mwana wa Mungu

Kama Mungu tayari amesha wahesabia haki yatokana na utakatifu tunaopata kutoka kwa Kristo, nani wetu bila sisi kulipia! Sio hati kuna jambo nzuri tuliolitenda, hama kwa vyovyote tupoteze. Kama Baba, Mungu anaweza kutuadhibu na anaadhibu watoto wake walio humu dunuiani, lakini wakati wote ubaki ni watoto wake (Mfano mwana mpotevu, Luka 15:24).

Mungu, tayari akiwa amewaesabia haki wale wasio wake, hataweza- na hawezi – kujichanganya mwenyewe kwa kuwalipa kwa mabaya. Warumi 8:34, Paulo anasema, “Ni nani atakayewahukumia adhabu?” Na hapo anapeana majibu manne, kila moja mahali pake tofauti ndani ya maandiko, lakini yote yamewe kwa pamoja hapa kueleza ulinzi wa aliyeamini usio na masharti.

1) Kristo alikufa;
2) Amefufuka;
3) Ni wakili wetu; na
4) Ni Mwombezi.

1) inategemea juu ya kifo chake kwa anjili yetu

Nani anayeweza kutuuhukumu kama adhabu imeshalipwa tayari? Thibitisho kuu ya ulinzi wetu wa milele ni kuhesabiwa haki kwa imani. Kuhesabiwa haki kwaonyesha vile Mungu anavyotuona sisi, sio vile wengine –ama hata sisi wenyewe –ujiona sisi. Hii kwa jumla ni jambo la kuangaliwa vile ilivyo (kisheria); Wakolosai 2:14 inasema ya kwamba “akiisha kuifuta” ile hati iliyoandikwa ya Kutushitaki kwa hukumu zake. “Imelipiwa kabisa” imekwisha! Wokovu huu ulikuwa na milele na milele wa mara moja na kabisa. Wokovu huu ulikuwa na milele na milele wa mara moja na kabisa.

2) Inategemea juu ya uhai wake kwa anjili yetu.

Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. Warumi 5:9-10. Kwa mifano mingine, angalia Warumi 5:19; 10:4’ Wakolosai 2:10 na zaidi.

3) Inategemea juu ya vile anafanya sasa: Utetezi na kana mwombezi wetu

Yesu ni pamoja na mtetezi na kuhani mwombezi. Naye kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai siku zote hili awaombee. Waebrania 7:25 “kuwaokoa kabisa” yamaanisha Akikisho kabisa kwangu!




Uaminifu wa Roho Mtakatifu

Utegemea juu ya Mungu Roho Mtakatifu

1) Juu ya kazi yake ya kufanya upya

Si kwa matendo ya haki tuliyoyatenda; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; Tito 3:5.
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama yamekuwa mapya 2 Wakorintho 5:17.

2) Juu ya kazi yake ya ubatizo

Maana sisi, tukiwa Wayahudi au watu wa mataifa mengine, watumwa au watu huru, sote tumebatizwa kwa Roho mmoja katika mwili huo mmoja; na sote tukanyweshwa Roho huyo mmoja. 1 Corinthians 12:13 1 Wakorintho 12:13

3) Juu ya kazi yake ya kutia muhuri

Naye ndiye aliye tutia muhuri, akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu. 2 Wakorintho 1:22 kutia muhuri: “tia muhuri”ilikuwa alama ya ulinzi (Mathayo 27:66, juu ya kaburi ya Kristo) na heshima. Wakati roho mtakatifu anatia muhuri, huwa na pete kama sahihi ya baba juu ya mioyo yetu. Yeye huweka alama ya heshima. Muhuri ulioharibika ni kuonyesha ulinzi usio kamilifu. Unaweza kuharibu muhuri? Shetani aweza?

Yeye ni ahadi ya kweli; ya kweli kabisa, ama ahadi, hili ni wazo la sheria. Ile ambayo hulinda mtu kuhusu lawama juu ya kitu kisichoharibiwa. Hili ni malipo, yaliyolipwa; kama ushahidi wa imani ya kweli, kuwa lazima kutimiza ahadi. Ahadi kama (A ahadi kama ilivyo Mwanzo 38:17)

Katika Warumi 8:23, Roho Mtaktifu anaonyeshwa kama malipo, “mazao ya kwanza,” ili kufuatwa na wengi. Tumetiwa mihuri hadi siku hiyo. Kama kuna mtu yeyote aliyezaliwa ya pili ndani ya Kristo na akatae kwenda mbinguni akifa, basi Mungu atakua amevunja ile ahadi yake. Hakuna masharti yametajwa. Ni kazi ya Mungu na inamtegemea yeye pekee. Ni thibitisho ya ina gani tunaweza kuwa nayo ya ushahidi? Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je ni dhiki, au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Warumi 8:35

Mtume Paulo ameorodhesha mambo saba yale aliyeamini uenda akayapitia yale wengine uenda wakafikiri yatakuja kati ya Mkristo na upendo wa Kristo (Paulo aliyapitia haya yote).

1) Dhiki: “Msukumo au dhiki”; yametajwa mara kwa mara na Paulo katika 2 Wakorintho);

2) Dhiki: Kumaanisha “Wembamba” kama kufinyiliwa, kukunjwa, usipofumua vuzuri sababu ya umati;

3) Adha: Imerudiwa mara 10 kwa Agano Jipya, mara yote inamaanisha injili.

4) Njaa: Imerudiwa mara 12 ndani ya Angano Jipya. Mungu wa Elija ujali walio wake.

5) Uchi: tazama 1 Wakorintho 4:11.

6) Hatari [penye hatari, hatari]: ]: Imerudiwa mara nane kwa mstari mmoja [2 Wakorintho 11:26; na 1 Wakorintho 15:30).

7) Upanga. Ulimwengu uchukia wenye haki.

Haya mambo -yanavyoonyesha makali yake – hayawatenganishi Wakristo na Kristo, badala yake ni sehemu ya “membo yote” (Warumi 8:28) Mungu ayatumia ili tuweze kumtii mwana wake. Lakini, katika mambo haya yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Warumi 8:37.






Uhuru wa ‘kusongea karibu’ kwa sababu ya maana ya UPENDO na kukubaliwa,
Na maisha mapya, nguvu zinazogeuza na mwanzo wa matumaini yetu.





Inategemea Mungu
ama

Inatengemea madhumuni yako mazuri.






Watoto wa mungu ni, kulingana na bibilia, wameokolewa daima na kulindwa milele:

  1. Wamezaliwa, tena na begu isiyohabirika ile inayozaa matunda ya milele ya uzima (1 Petro 1:23)
  2. Wanasimama mbele za Mungu na mavazi (yanayometameta) wataktfifu wa Kristo, na sio kwa anjili yao (2 Wakorintho 5:21; Warumi 5:19-21)
  3. Kondoo wake wampewa Maisha milele –hawatapotea (Yohana 10:28).
  4. Uhai wao umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu (Wakolosai 3:1-3).
  5. Tayari wanaishi maisha ya mbinguni ndani ya Kristo (Waefeso 1:3; 2:6).
  6. Adhabu yao ya dhambi imesha milele tatuliwa kupitia kazi kamilifu ya msalaba ya Bwana wetu Yesu Kristo (Warumi 4:23-5:2; 5:6-9).
  7. Kupoteza dhawabu mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo ni dhairi kwa Wakristo wasiojali, lakini sio kupoteza wokovu (1 Wakorintho 3:10-15).
  8. Mungu kwa uaminifu wake awapiga watoto wake wote, hata umubidi kuwachukua nyumbani wale wanaokataa kutii marekebisho yake (Waebrania 12:6-11; 1 Wakorintho 5:1-5; 11:28-32).
  9. Tayari wameisha okolewa kutoka kwa gadhabu itakayokuja (1 Wathesolonike 1:9, 10; 5:8-10).
  10. Walitiwa muhuri na Roho Mtakatifu hata siku ya ukombozi (Waefeso 4:30; Warumi 8:23).
  11. Bwana anawajua walio wake; waalimu wa uongo watafichuliwa siku ile mbele ya kiti cha enzi (2 Timotheo 2:19; Ufunuo 20:11-15; Mathayo 7:21-23)
  12. Mungu ndiye anayeanzisha kazi nzuri kwa yule anayeamini, amehahidi atatimiza hata siku ya Kristo Yesu; “inawastahili wafanye kazi” sio “kufanyia wokovu wao kazi” (Wafilipi 1:6; 2:12, 13).
  13. Tayari wao ni mawe yaliyo hai, ya kugwa mwe nyumba ya Roho ambaye Kristo mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. (1 Petro 2:5’ Waefeso 2:20-22).
  14. Wao ni viungo vya mwili wa Kristo, kila moja na kazi yake na pakiwa mmoja aliko basi mwili sio kamilifu. (1 Wakorintho 12:12-27).
  15. Wanalindwa na nguvu za Mungu, kwa njia ya imani, sio kwa juhudi ama kazi ya yule ameokolewa. (1 Petro 1:5).
  16. Urithi usioharibika, urithi wa milele umeifadhiwa tayari na Mungu (1 Petro 1:1-4).
  17. Wao ni zawadi isiyoweza kufutiliwa mbali ya Mungu Baba kwa Mungu Mwana (Yohana 17:6,7).
  18. Kurudi nyuma ni dhambi, lakini damu ya Yesu Kristo, Mwana w Mungu, hutusafisha sisi kutoka kwa dhambi zote (1 Yohana 1:7-9)
  19. Aweza kuwaokoa kabisa kwa maana Kristo “yu hai siku zote ili awaombee” (Waebrania 7:25).
  20. Wako ili kumwamini Kristo “ametuneemesha katika huyo mpendwa” (Waefeso 1:6).
  21. Wala chote hakitaweza kuwatenga na upendo wa Kristo. (Warumi 8:38-39).
  22. Kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa (Waebrania 10:10-14).
  23. Hawawezi kuwa hawajazaliwa (Yohana 3:6-8)
  24. Kristo anakaa ndani yao hata milele (2 Yohana 2).
  25. Hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba, na hii inamaanisha Mkristo aliyeokoka. (Yohana 10:29).
  26. Wale wote aliowatakasa mwishowe atawatukuza – hakuna yeyote atakayopotea kwa njia. (Warumi 8:28-30).
  27. Ndani ya miili yao halikai neno njema; wameokolewa kwa neema (huruma isiyowasitairi) na sio kwa matendo yao (Waefeso 2:8,9).
  28. Kipawa na mwito wa Mungu, haziwezi kurudishwa nyuma; Mungu hataweza kufutilia mbali ahadi zake wala yeyote ajaye kwake kupitia kwa Krsito hatamtupa nje kamwe (Warumi 11:29; John 6:37; 17:2).




Swali ya umuhimu tumeshaisikia

Siwezi kuiamini!


Takatifu B. Mbuzi


  Lakini!.....Lakini!.....Lakini!... Lakiiiiniiii!
Na yule mtu, unayemjua na “ameokoka”, lakini sasa, unajua amerudia maisha ya dhambi, na mambo ya kiajabu anakusudia kutenda. Na ikiwa wata “mwua” mtu ama _bla__bla (jaza pengo)???

Swali KAMILI unayojaribu kuuliza hapa ingekuwa: ni kwa nini Mungu akakubali waokoke kwanza(“kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu. (Waefeso 2:8-9). Ikiwa Mungu alijua vile huyu “mtu”atakuwa baadaye yule unayemjua, atakachotenda, na awaokoe! Basi!! Usimurukie huyo mtu ukienda mbinguni, watakapolalamika kama kuna “neema nafuu” ama umashuhuri wa neema kw nguvu ya
“Damu ya Yesu”


. Wakati Yesu aliposuribiwa Msalabani karibu miaka 2000 iliyopita, alikuwa ATIMAYE sadaka. Sadaka ya damu kweli kweli.
· Alichumbuliwa kwa maovu yetu,
· Ndevu zake ziling’olewa kutoka kwa mashavu yake,
· Kichwa chake kilidungwa na taji yamiiba,
· Alipigwa uso wake vibaya sana. Hangetambulika. Biblia inasema aliteswa kuliko mtu mwingine YEYOTE.
· Mikono na miguu yake ilipigiliwa na makali ya vyuma vyembamba.
· Ubavu wake ulichomwa kwa mkuki, baadaye akafa.

Hii sio jambo kwangu kwa kuichukulia “rahisi”



Mungu ndiye pekee anayeweza kuona maisha toka mwanzo hadi mwisho.



Na kama ilimpendeza Yesu “kuwakomboa” hata wao pia, sitaweza kulalamika.
Kama macho yako yamtazama YEYE, hayako kwao
Wacha upendo wake kwako, ikuvute wewe KWAKE.

  Fungua Biblia

Yampiga Shetani