Articles of Faith in Swahili


Mambo ya kuamini

 1. Ya Biblia: Ni lenye pumzi ya Mungu na Ulinzi
 2. Ya Mungu wa Kweli
 3. Ya Roho Mutakatifu
 4. Ya Ibilisi au shetani
 5. Ya Maumbile
 6. Ya Kuanguka kwa mtu
 7. Ya kuzaliwa na Bikira
 8. Ya kusamehewa Dhambi
 9. Ya Nehema kwa kuzaliwa upya
 10. Wokovu Kasisa ni Kipawa cha Mungu
 11. Ya Kuhesabiwa haki
 12. Ya kutubu na Imani
 13. Ya Kanisa
 14. Ya ubatizo na Meza la Bwana
 15. Ya Saburi ya Watakatifu
 16. Ya wenye Haki na Wasio Haki
 17. Ya Serikali
 18. Ya ufufuo na Kurudi kwa Kristo na Matokeo ya Baadaye
 19. Ya Umisheni
 20. Nehema ya Kupeana
1. Ya Biblia: Ni lenye pumzi ya Mungu na Ulinzi

Tunaamini ya kwamba Biblia takatifu limeandikwa na wanadamu wakiongonzwa n Roho mtakatifu; na kwa hivyo ina ukweli usiochanganyika na makosa yeyote yale. Na kwa hivyo ni, na itabaki kuwa siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Ile pekee ndio kamilifu na ufunuo wa mwisho wa mapenzi ya mungu kwa binadamu; hiyo ndio upatanishi ya kweli ya ushirika wa Wakristo na mamulaka makuu ya kuongoza tabia za binadamu; makubaliano yao na maoni yao pia.

 1. Na “Biblia Takatifu” tunamaanisha vitabu vyote sitini na sita, kutoka mwanzo hadi ufunuo, ile kama vile ilivyoandikwa kutoka mwanzo sio tu inaonyesha ndio neno la Mungu, bali NI Neno la Mungu.

 2. Na “pumzi ya Mungu” tunamaniisha ya kwamba vitabu vya ‘’biblia vimeandikwa na watu watakatifu wa kale, kama walivyo ongozwa na Roho Mtakatifu, kwa hivyo uandishi wao ulikuwa sio wakibinadamu bali wa muongozo wa Mungu uliwaongoza kuandika kila neno pasipokuwa na makosa yeyote, kinyume na uandishi mwingine wowote ulioandikwa ama utakaoandikwa.

 3. Hivyo Biblia pekee ya Kingereza yenye kukubalika hapa duniani naya kweli kabisa ni inayoitwa King James Version. Hiyo ndio pekee wenye kuongea Kingereza Duniani wanastahiri kuisoma kama neno la Mungu. Mungu alisema atalinda neno lake kwa hivyo neno la Mungu ni la kwa kweli uamini ama usiamini.

Zaburi 19:7-11
7. Sheria ya Bwana ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, Humtia mjinga hekima.
8. Maagizo ya Bwana ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya Bwana ni safi, Huyatia macho nuru.
9. Kicho cha Bwana ni kitakatifu, Kinadumu milele. Hukumu za Bwana ni kweli, Zina haki kabisa.
10. Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali.
11. Tena mtumishi wako huonywa kwazo, Katika kuzishika kuna thawabu nyingi.

Zaburi 119:89
Ee Bwana, neno lako lasimama Imara mbinguni hata milele.

Zaburi 119:105
Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.

Zaburi 119:30
Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga.

Zaburi 119:160
Jumla ya neno lako ni kweli, Na kila hukumu ya haki yako ni ya milele.

Mithali 30:5-6
5. Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.
6. Usiongeze neno katika maneno yake; Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.

Mithali 8:20
Natembea katika njia ya haki, Katikati ya mapito ya hukumu.

Luka 16:31
Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.

Luka 24:25-27
25. Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!
26. Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?
27. Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.

Luka 24:44-45
44. Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.
45. Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.

Yohana 5:39
Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.

Yohana 5:45-47
45. Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi.
46. Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu.
47. Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?

Yohana 12:48
Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.

Yohana 17:17
Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.

Matendo ya Mitume 1:16
Ndugu, ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi, katika habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu;

Matendo ya Mitume 28:25
Na walipokuwa hawapatani wao kwa wao, wakaenda zao, Paulo alipokwisha kusema neno hili moja, ya kwamba, Roho Mtakatifu alinena vema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya,

Warumi 3:4
Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu.

Warumi 15:4
Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.

Waefeso 6:17
Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;

2 Timothy 3:16-17
16. Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
17. ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.

I Petro 1:23
Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.

2 Petro 1:19-21
19. Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
20. Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
21. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Ufunuo 22:19
Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.

2. Ya Mungu wa Kweli

Tunaamini ya kwamba kuna mmoja, na mmoja kabisa, anayeishi na Mungu na Mungu wa kweli, asiyekuwa na kipimo, Roho anayechunguza aliyeumba vyote na mwenye mamlaka yote Mbinguni na duniani, mtukufu kwa utukufu na anayestahili sifa zote, kumuamini na kumpenda; na kwa pamoja kuamini utatu wa Mungu, Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Wote wako sawa kwa kila jambo la utakatifu, wakitekeleza kazi zao kila moja anapostahili kwa kazi kubwa ya wokovu kupitia kwa Damu ya Kristo aliyemwaga damu kwa ajili yetu

Mwanzo 17:1
Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.

Kutoka 20:2-3
2. Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
3. Usiwe na miungu mingine ila mimi.

Kutoka 15:11
Ee Bwana, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?

Zaburi 83:18
Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.

Zaburi 90:2
Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.

Zaburi 147:5
Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu, Akili zake hazina mpaka.

Yeremia 10:10
Bali Bwana ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake. Mathayo 28:19
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

Markoo 12:30
nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.

Yohana 4:24
Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Yohana 10:30
Mimi na Baba tu umoja.

Yohana 15:26
Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.

Yohana 17:5
Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

Acts 5:3-4
3. Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?
4. Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.

Warumi 11:23
Na hao pia, wasipokaa katika kutokuamini kwao, watapandikizwa; kwa kuwa Mungu aweza kuwapandikiza tena.

I Wakorintho 8:6
lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo.

I Wakorintho 12:4-6
4. Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.
5. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.
6. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.

I Wakorintho 12:10-11
10. na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;
11. lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.

2 Wakorintho 13:14
Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.

Waefeso 2:18
Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja.

Waefeso 4:6
Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.

Wafilipi 2:5-6
5. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
6. ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;

I Timothy 1:17
Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.

I Yohana 5:7
Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.

Ufunuo 4:11
Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.

3. Ya Roho Mutakatifu

Tunaamini ya kwamba Roho ni Mtakatifu; yeye ni sawa na Mungu Baba na Mungu Mwana na jinsi walivyo wao wote ni sawa; ya kwamba alishiriki kwa kuumba viumbe; kwamba kwa usiano wake na watu wasioamini, anawarudisha kwa njia ya wokovu mpaka kusudi la mungu linatimilika maishani mwao; anaakikisha kwa habari ya dhambi, na hukumu na haki’ yeye ni shahidi wa ukweli wa injili kwa mahubiri na ushuhuda, kwamba ndiye muwakilishi wa kuzaliwa upya; kwamba ndiye wa kutia muhuri; kwamba anaongoza, anafunza, anashuhudia, anatakasa, na kusaidia Mkristo. Lakini hatuamini ya kwamba Roho mtakatifu ni mgeni wa kutisha. Tunaamini ya kwamba Roho Mtakatifu yu hai nayu agali akihudumia mioyo ya wateule wa Mungu.

Wakati ule mtu anapoweka imani yake kumwamini Yesu Kristo, hapo ndipo Roho Mtakatifu anapoingia kukaa ndani yake.

Mathayo 3:11
Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Mathayo 28:19
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

Markoo 1:8
Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.

Luka 1:35
Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.

Luka 3:16
JYohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto;

Luka 24:49
Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.

Yohana 1:33
Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.

Yohana 3:5-6
5. Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
6. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

Yohana 14:16-17
16. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
17. ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

Yohana 14:26
Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Yohana 15:26-27
26. 26 Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.
27. Nanyi pia mnashuhudia, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwapo pamoja nami.

Yohana 16:8-11
8. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
9. Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;
10. kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena;
11. kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.

Yohana 16:13
Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

Matendo ya Mitume 5:30-32
30. Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambaye ninyi mlimwua mkimtundika katika mti.
31. Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.
32. Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio.

Matendo ya Mitume 11:16
Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji kweli, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.

Warumi 8:14
14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu..

Warumi 8:16
Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;

Warumi 8:26-27
26. Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
27. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

Waefeso 1:13-14
13. Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.
14. Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.

2 Wathesalonike 2:7
Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.

2 Wathesalonike 2:13
Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;

Waebrania 9:14
basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?

I Petro 1:2
kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.

4. Ya Ibilisi au shetani

Shetani ndiye aliyekuwa malaika maridadi aliyeumbwa na Mungu lakini alijiamulia kuwa kama Mungu. Kwa kiburi chake na ukatiri wake akatupwa na Bwana akamtengenezea mahali (Jehanamu) akatupwa hata nchi, na Malaika wake wakatupwa pamoja naye. Sasa wataishi ndani ya shimo la kuzimu na baadaye Jehanamu milele. Kwa sasa ni mfalme wa uwezo wa anga, roho Yule atendaye kazi sasa katika Wana wa kuasi. Tunamchukulia kuwa ndiye mjaribu wa binadamu, adui wa Mungu na Kristo, Mshitaki wa watakatifu, mwanzilishi wa deni za uongo, nguvu zote za ngiza, mwisho wake ni kushindwa mikononi mwa Mwana wake Mungu, na hukumu ya milele Jehanam. Ibilisi sio mwenye nguvu zote hama yuko kila mahali mara moja, hawezi kuwa mahali zaidi ya moja saa moja. Shughuli zake utegemea mipaka na vipimo alivyowekewa. Mungu wetu ni mwenye nguvu zote.

Isaya 14:12-15
12. Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!
13. Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota
14. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.
15. Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo

Ezekieli 28:14-17
14. Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.
15. Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.
16. Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.
17. Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama..

Mathayo 4:1-3
1. Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.
2. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.
3. Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.

Mathayo 13:25
lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.

Mathayo 25:41
Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

Mathayo 27:39
Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisa-tikisa vichwa vyao, wakisema,

Markoo 13:21-22
21 Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki;
22 kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule.

Luka 22:3-4
3 Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara.
4 Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao.

Yohana 14:30
Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.

Waefeso 2:2
ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;

2 Wakorintho 11:13-15
13. Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.
14. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
15. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.

1 Wathesalonike
Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida.

2 Wathesalonike 2:8-11
8. Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
9. yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
10. na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11. Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;

1 Petro 5:8
Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.

2 Petro 2:4
Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;

1 Yohana 2:22
Ja miriambo to kara en ng'a? En ng'ama wacho ni Yesu ok en Kristo. Jalno e Jasik Kristo, nikech odagi Wuoro kaachiel gi Wuowi.

I Yohana 3:8
atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.

I Yohana 4:3
Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.

2 Yohana 7
For many deceivers are entered into the world, who confess not that Jesus Christ is come in the flesh. This is a deceiver and an antichrist.

Jude 6
Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.

Ufunuo 12:7-10
7. Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
8. nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
9. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
10. 10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.

Ufunuo 13:13-14
13. Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.
14. Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.

Ufunuo 19:11
Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.

Ufunuoe 19:16
Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana.

Ufunuo 19:20
Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;

Ufunuo 20:1-3
1. Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
2. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;
3. akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.

Ufunuo 20:10
Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.

5. Ya Maumbile

Tunaamini mambo ya Mwanzo vile Mungu alivyoumba viumbe na yote Mungu aliyoyatenda kwa kuumba vyote. Yote haya tunasitahiri kuyatafsiri jinsi ilivyoandikwa kwa kitabu cha Mwanzo na si kwa kutafsiri kwa vingine vyovyote; kwamba mtu aliumbwa na mfano wa Mungu; Kwamba sio mnyama aliyegeuka kuwa binadamu, ama binadamu kutokezea kwa njia zingine za kisayansi; kwamba wanyama na majani zilitokeza kwa Amri ya Mungu, kwa jinsi zake; na kwa kuwa Mungu aliumba binadamu mume na mke, tunaamini ya kwamba ndoa ya halisi inastahili kuwa ya mume na mke, aliamuru ya kwamba hakuna ruhusa ya mapenzi inje ya ndoa. Tunaamini ya kwamba mashoga, mapenzi ya wanawake kwa wao wenyewe, mapenzi ya binadamu na wanyama, mapenzi ya watu wa jamii moja, usherati, usizi, picha za ngono, yote haya ni matumizi mabaya ya zawadi nzuri ya Mungu aliyetupa ya kufanya mapenzi. Tunaamini ya kwamba ni hatia mbele za Mungu mtu kujigeuza kwa maumbile yake kwa njia yeyote ile aonekane vingine kinyume na alivyoumbwa.

Sisi hatuamini mafundisho ya kwamba Mungu aliumba vitu kwa miaka mingi; akaumba Dunia, akapumzika kwa miaka, tena akaumba mbingu, akapumzika kwa miaka, kila kitu Mungu aliumba na ikamchukua miaka mingi kwa kupumzika. Kuna watu wengi wanaoamini hayo, sisi hapa Amazing Grace Baptist Church hatuamini hayo. Tunaamini Mungu aliumba vitu vyote kwa siku sita mfululizo na siku ya saba akapumzika.

Mwanzo 1:1
Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

Mwanzo 1:11
Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.

Mwanzo 1:24
Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.

Mwanzo 1:26
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

Mwanzo 1:27
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Mwanzo 2:21
Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,

Mwanzo 2:22
na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu

Mwanzo 2:23
Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.

Kutoka 20:11
Ee Bwana, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?

Nehemia 9:6
Thou, even thou, art LORD alone; thou hast made heaven, the heaven of heavens, with all their host, the earth, and all things that are therein, the seas, and all that is therein, and thou preservest them all; and the host of heaven worshippeth thee.

Yeremia 10:12
12 Ameiumba dunia kwa uweza wake, Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake, Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.

Yohana 1:3
Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.

Matendo ya Mitume 4:24
To kane joma oyie owinjo wachgino, ne git-ing'o dwondgi malo riat ka gilamo Nyasaye ni, "Aa Ruoth Nyasaye Manyalo Gik Moko Duto, In ema nichweyo polo gi piny gi nam koda ka gik moko duto manie igi.

Matendo ya Mitume 17:23-26
23. Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua.
24. Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;
25. wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.
26. Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;

Warumi 1:20
Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru;

Wakolosai 1:16-17
16. Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
17. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.

Waebrania 11:3
Yie ema miyo wayango ni Wach Nyasaye ema nochweyo gik moko duto manie polo gi piny, mi nomiyo gik mantie mineno gi wang' owuok kuom gik maok ne.

Ufunuo 10:6
akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya;

6. Ya Kuanguka kwa mtu.

Tunaamini ya kwamba mtu aliumbwa bila dhambi chini ya sheria ya muumba wake, lakini kwa dhambi ya kujitakia akaanguka kutoka kwa utakatifu na maisha ya Raha, matokeo yake ni kwamba sasa binadamu wote ni wenye dhambi, sio kwa kushurutishwa bali kwa kujitakia; na kwa hivyo yuko chini ya hukumu bila tetezi au sababu. Tuna laana ya dhambi na kifo juu ya vichwa vyetu na Roho zetu kwa sababu ya kutokutii kwa hihari kwetu kwa yale Mungu alikuwa ametuagiza kutenda tunaendelea kuishi kwa mazingira ya familia hiyo isiyotii maangizo ya Mungu.

Mwanzo 3:1-6
1. Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
2. Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
3. lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
4. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
5. kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
6. Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.

Mwanzo 3:24
Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.

Ezekieli 18:19-20
19. Lakini ninyi mwasema, Kwani yule mwana asiuchukue uovu wa baba yake? Yule mwana atakapofanya yaliyo halali na haki, na kuzishika amri zangu na kuzitenda, hakika ataishi.
20. Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.

Warumi 1:18
Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.

Warumi 1:20
Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru;

Warumi 1:28
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.

Warumi 1:32
ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.

Warumi 3:10-19
10. kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja.
11. Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu.
12. Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.
13. Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao.
14. Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.
15. Miguu yao ina mbio kumwaga damu.
16. Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao.
17. Wala njia ya amani hawakuijua.
18. Kumcha Mungu hakupo machoni pao.
19. Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu;

Warumi 5:12
Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;

Warumi 5:19
Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.

Wagalatia 3:22
Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.

Waefeso 2:1
Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;

Waefeso 2:3
ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.

7. Ya kuzaliwa na Bikira

Tunaamini ya kwamba Yesu alikuja kutimiza unabii wa Isaya wa Masii. Kwamba ndiye mwenye kutimiza hiyo ahadi. Kama vile Yohana Mpatizaji anavyosema. “Tazama Mwana-kondoo wa Mungu!”

Tunaamini ya Kwamba Yesu alizaliwa kwa nguvu ya Roho Mtakatifu kwa kiajabu; akazaliwa na Mariamu, bikira, jinsi vile hakuna Mwingine alizaliwa hivyo hata hakuna mwingine atazaliwa jinsi hiyo na mwanamke, na hivyo yeye ni mwana wa Mungu, na ni Mungu, mwana.

Mwanzo 3:15
nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.

Zaburi 2:7
Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.

Isaya 7:14
Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.

Mathayos 1:18-25
18. Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
19. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.
20. Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
21. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
22. Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,
23. Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
24. Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;
25. asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.

Marko 1: 1
Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.

Luka 1:35
Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.

Yohana 1:14
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

Wagalatia 4:4
Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,

I Wakorintho 15:47
Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni.

I Yohana 5:20
Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.

8. Ya kusamehewa Dhambi

Tunaamini wokovu wa wenye dhambi ni wa nehema; kwa upatanishi wa Mwana wa Mungu, ule kwa kupeanwa na Mungu Baba, Bila malipo alichukua mwili wa Binadamu, lakini Bila dhambi, akitii sheria kwa unyenyekevu wake, na kwa kifo chake akalete msamaha kamilifu wa dhambi zetu. Kifo chake hakikuwa hati anateswa kutetea imani; bali alikuwa anasimama mahali pa mwenye dhambi kuteswa na kufa kwa anjili ya dhambi zetu. Mwenye haki kufa kwa ajili ya wenye dhambi, Kristo, Bwana, yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti. Ili kwa ufufuo wake kutoka kwa wafu, aliketi mkono wa kiume wa ukuu huko juu, amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao. Sasa yeye ndio kwa vyovyote vile anastahili kuwa mwenye huruma na Mwokozi awezaye.

Isaya 53:4-7
4. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
5. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
6. Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.
7. Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.

Isaya 53:11
11. Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.
12. Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.

Mathayo 18:11
Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea.

Yohana 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Yohana 10:18
Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.

Matendo ya Mitume 15:11
Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.

Warumi 3:24-25
24. wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
25. ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa.

Wagalatia 1:4
ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu.

Waefeso 2:8
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;

Wafilipi 2:7-8
7. bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
8. tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Waebrania 2:14
To kaka nyithindo nigi ringruok gi remo e kaka en bende nokawo kidono, mondo kuom thone oketh teko marjal man-gi teko mar tho, ma en Jachien,

Waebrania 7:25
Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

Waebrania 9:12-15
12. wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.
13. Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili;
14. basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?
15. Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.

Waebrania 12:2
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

9. Ya Nehema kwa kuzaliwa upya

Tunaamini ili kuzaliwa upya, wenye dhambi lazima kuzaliwa upya; hivyo kuzaliwa upya ni kuumbwa upya ndani ya Kristo Yesu; Yaani wokovu ni mara moja lakini sio kila mara’ hivyo kwa kuzaliwa upya mwenye kufa kwa dhambi anafanyika kiumbe kipya na kupokea maisha ya milele zawadi ya bure ya Mungu, ni kuumbwa jinsi ile inazidi mafikira na maelezo yetu. Sio kwa utamaduni, ama tabia, ama kwa mapenzi ya mtu, lakini yote kwa njia ya pekee na nguvu za Roho Mtakatifu na neno la kweli ili tuweze kutii na kulinda injili ya kweli.

Luka 5:27
Baada ya hayo akatoka, akaona mtoza ushuru, jina lake Lawi, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate.

Yohana 1:12-13
12. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
13. waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

Yohana 3:3
Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.

Yohana 3:6
Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

Yohana 3:7
Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.

Matendo ya Mitume 2:41
Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.

Warumi 6:23
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu..

2 Wakorintho 5:17
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

2 Wakorintho 5:19
yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.

Wagalatia 5:22
Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,

Waefeso 2:1
Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;

Waefeso 5:9
kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli;

Wakolosai 2:13
Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote;

1 Yohana 5:1
Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye.10. Wokovu Kasisa ni Kipawa cha Mungu

Tumaanini wokofu ni kwa kuchanguliwa na Mungu kwa nehema. Ili Baraka ya wokovu iwe bila malipo kwa njia ya injili; huu ni wajibu wa wote kuchukua kwa upendo, na kutubu, na imani na kutii; na hakuna chochote kinachoweza kuzuia mwenye dhambi kuokolewa isipokuwa yeye kukataa injili kwa kujitakia. Kukataa ambako kutazidisha hukumu yake siku ya kiama. Ni raisi mtoto anaweza kuamini ata wewe unaweza. Kipawa ni bila malipo. Kuipata ni kuwa na matumaini.

Isaya 55:1
Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila thamani.

Mathayo 11:28
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Yohana 3:15-18
15. ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.
16. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
. 17. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
18. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

Yohana 3:36
Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

Yohana 5:40
Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima.

Yohana 6:37
Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.

Matendo ya Mitume 2:38
Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Warumi 8:29-30
29. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.
30. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.

Warumi 10:13
kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.

I Wakorintho 15:10
Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.

Waefeso 2:4-5
4. But God, who is rich in mercy, for his great love wherewith he loved us,
5. Even when we were dead in sins, hath quickened us together with Christ, (by grace ye are saved;)

Wakolosai 3:12
Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,

I Thesalonika 1:4
Kwa maana, ndugu mnaopendwa na Mungu, twajua uteule wenu;

I Timotheo 1:15
Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.

Tito 1:1
Paulo, mtumwa wa Mungu, na mtume wa Yesu Kristo; kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli ile iletayo utauwa;br>
Tito 3:5
si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;

Isaya 64:6
Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.

I Petro 1:2
kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.

Ufunuo 22:17
Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.

11. Ya Kuhesabiwa haki

Tunaamini ya kwamba Baraka kubwa ya injili ile Yesu anawapa wanao mwamini ni kuhesabiwa haki, kuhesabiwa haki huko kunashirikisha msamaha wa dhambi, na kipawa cha maisha ya milele kwa kuishi maisha ya utakatifu; wala si kwa matendo mema tuliyotenda; lakini kwa imani pekee kwa damu ya Mwokozi, tunawekelewa utakatifu wake juu yetu.

Isaya 53:11
Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.

Habakuki 2:4
Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.

Zekaria 13:1
Katika siku hiyo watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi kwa dhambi na kwa unajisi.

Matendo ya Mitume 13:39
na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa.

Warumi 1:11
Kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapa karama ya rohoni, ili mfanywe imara;

Warumi 4:1
Basi, tusemeje juu ya Ibrahimu, baba yetu kwa jinsi ya mwili?

Warumi 5:1-9
1. Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
2. 2 ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.
3 Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi;
4. na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini;
5. na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.
6. Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.
7. Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema.
8. Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.
9. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.

Warumi 8:1
Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

Wagalatia 3:11
Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani.

Tito 3:5-7
5. si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;
6. ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu;
7. ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.

Waebrania 10:38
Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.

12. Ya kutubu na Imani

Tunaamini ya kwamba kutubu na imani ni mambo yanayobidi niya lazima, na nehema sizizotenganishwa ambazo zimewekwa mioyoni mwetu na Roho Mtakatifu wa Mungu, ambapo tunapojihisi kuwa wenye makosa hatari na wanyonge, na kwa njia ya wokovu kupitia kwa Kristo, tumurudie Mungu na mioyo yenye kuuzunishwa na dhambi, kutubu na kusali kwa nehema; na saa hiyo ndani ya moyo kumpokea Bwana Yesu Kristo na atharani kumukiri yeye kama Mwokozi wetu wa pekee na Mwokozi anayetutosha.

Zaburi 51:1-4
1 Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.
2 Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu.
3 Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima.
4 Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.

Zaburi 51:7
Purge me with hyssop, and I shall be clean: wash me, and I shall be whiter than snow.

Isaya 55:6-7
6. Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri,
7. Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji

Marko 1:15
akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.
Luka 12:8
Nami nawaambia, kila atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu;

Luka 18:13
Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.

Matendo ya Mitume 2:37-38
37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Matendo ya Mitume 20:21
nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo.

Warumi 10:9-11
9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
11 Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika.

Warumi 10:13
kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.

13. Ya Kanisa

Tunaamini ya Kwamba Kanisa la Ubatizo ni Washirika Walioamini na wakabatizwa kulingana na Agano la imani na ushirika wa injili, Kanisa linalojulikana kuwa juu na kwakueneza habari njema ya nehema; linalozingatia sana maagizo yote yanayousiana kulingana na neno lake; kwamba watumishi wake ni maaskofu, ama mashemasi wale kuhitimu kwao, madai yao, na wajibu unaowasitahili unaelewa vizuri ndani ya Biblia.

Tunaamini ya kwamba wanaume na wanawake kwa mambo ya kiroho wote ni sawa mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini Mungu ametenganisha kazi wanaostahili kutenda nyumbani na Kanisani. Mwanaume ndiye anastahili kuwa kiongozi wa Nyumba, na wanaume ndio wanaofaa kushikilia nyathifa Kanisani(Maaskofu na Mashemasi). Kulingana na vile ilivyo, ni wanaume pekee wanaostahili kupewa vyeti vya kutawaswa na Kanisa.

Tunaamini kazi kubwa ya Kanisa inapatikana ujumbe mkuu wa Yesu “Basi enendeni: kwanza, kuwafanya watu wanafunzi wake; pili, kulijenga Kanisa, tatu, kufunza na kushauri kulingana na maagizo yake. Hatuamini kinyume na mpangilio huyu, tunaamini kanisa lenyewe lina haki ya kujipangia mipango yake bila ushawishi wowote, huru kabisa kutokana na utawala wa juu wa watu ama mashirika; na kwa hivyo Yule pekee ndiye kiongozi ni Kristo kwa njia ya Roho Mtakatifu; kwamba ni kulingana na Biblia Makanisa ya kweli kuungana pamoja kushindania imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tunatangaza injili; kwamba kila Kanisa ndio pekee lenye kujipangia mipango yake ya maendeleo. Kuhusu mambo yote ya washirika ya mipangilio ya uongozi, ya kurekebisha tabia, na ya kupeana misaada, Mahamuzi ya Kanisa ndio mwisho. Kila Kanisa yenye kuajibika kwa mipangilio yake na ndio yenye kuajiri na kufuta.

Mambo ya Walawi 27:31
Na kama mtu akitaka kukomboa cho chote cha zaka yake, ataongeza sehemu yake ya tano juu yake.

Malaki 3:10
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

Mathayo 28:19-20
19. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20. na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Matendo ya Mitume 2:41-42
41. Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.
42. Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.

Matendo ya Mitume 6:5-6
5. Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia;
6. Ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao.

Matendo ya Mitume 14:23
Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.

Matendo ya Mitume 15:22-23
22. Basi ikawapendeza mitume na wazee na kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba; nao ni hawa, Yuda aliyeitwa Barsaba, na Sila, waliokuwa watu wakuu katika ndugu. Wakaandika hivi na kupeleka kwa mikono yao,
23. Mitume na ndugu wazee, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shamu na Kilikia, walio wa Mataifa; Salamu.

Matendo ya Mitume 20:17-28
17. Toka Mileto Paulo akatuma watu kwenda Efeso, akawaita wazee wa kanisa.
18. Walipofika kwake, akawaambia, Ninyi wenyewe mnajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu wakati wote,
19. nikimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, na kwa machozi, na majaribu yaliyonipata kwa hila za Wayahudi;
20. ya kuwa sikujiepusha katika kuwatangazia neno lo lote liwezalo kuwafaa bali naliwafundisha waziwazi, na nyumba kwa nyumba,
21. nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo.
22. Basi sasa, angalieni, nashika njia kwenda Yerusalemu hali nimefungwa rohoni, nisiyajue mambo yatakayonikuta huko;
23. isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja.
24. Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu.
25. Na sasa, tazameni, mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko, hamtaniona uso tena.
26. Kwa hiyo nawashuhudia wote siku hii ya leo, ya kuwa mimi sina hatia kwa damu ya mtu awaye yote.
27. Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu.
28. Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.

I Wakorintho 5:11-13
11. Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.
12. Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani?
13. Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu.

I Wakorintho 6:1-3
1. Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu?
2. Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?
3. Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?

I Wakorintho 11:2
Basi nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea.

I Wakorintho 12:4
Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule..

I Wakorintho 12:8-11
8. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;
9. mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;
10. na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;
11. lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.

I Wakorintho 16:1-2
1. Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo.
2. Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;

Waefeso 1:22
akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo

Waefeso 4:11
Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;

Waefeso 5:23-24
23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.

Wakolosai 1:18
Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.

1 Timotheo 3:1-13
1. Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema.
2. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;
3 si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;
4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; ,
5 yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?
6 Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.
7. Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.
8. Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana,si watu wanaotamani fedha ya aibu.
9. wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi.
10. Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia.
11. Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.
12. Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao.
13. Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu.

14. Ya ubatizo na Meza la Bwana

Tunaamini ya kwamba ubatizo wa Mkristo unastahili kuwa wa kutumbukizwa kichwa ndani ya maji kwa Yule anaye amini, kwa jina la Baba, la Mwana na Roho Mtakatifu. Kwa mamulaka ya Kanisa, Kuonyesha kwa utiifu umaridadi wa imani yetu ndani ya Yule aliyesurubiwa, akazikwa, na mwokozi aliyefufuka ikimaanisha ya kwamba sisi tumekufa kwa dhambi na kufufuka kuishi maisha mapya, ya kwamba hiyo ni jambo la lazima ya Kanisa kutekeleza pamoja na kushiriki meza ya Bwana, ambapo washiriki wa Kanisa, kwa kutumia mkate na uzao wa mzabibu waonyesha kifo cha upendo cha Kristo; hii inatunguliwa na mtu kujitafakari mwenyewe na kisha kupokea, hii inastahili kuwa maji ya uzao wa mzabibu inayomaanisha damu safi ya Kristo iliyomwangwa kwa anjili yetu. Mkate kumaanisha mwili wa Kristo ulioteswa kwa ajili yetu.

Mathayo 3:6
naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao.

Mathayo 3:16
Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;

Mathayo 28:19-20
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Yohana 3:23
Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa

Matendo ya Mitume 2:41-42
41. Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.
42. Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.

Matendo ya Mitume 8:36-39
36. Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe?
37. Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.
38. Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza.
39. Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi.

Warumi 6:3-5
3. Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?
4. Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
5. Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;

I Wakorintho 11:23-28
23. Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate,
24. naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.
25. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.
26. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.
27. Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.
28. Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.

Wakolosai 2:12
Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.

15. Ya Saburi ya Watakatifu

Tunaamini ya kwamba tu ni wale Wakristo wakweli wanaostahili kuvumilia hadi mwisho; kwamba wajibu wa kuvumilia kwao kwa anjili ya Kristo ni thihirisho ya kwamba hawako chini ya usimamizi wa yeyote ila tu imani na kupenda Bwana kunawaweka salama kwa vita vya imani, na kwa hivyo wanalindwa na nguvu za Mungu kwa imani hadi wokovu wa milele, kwamba hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wa Mungu.

Zaburi 121:3
Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye;

Mathayo 6:20
bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;

Mathayo 13:19-21
19. Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo
20. Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno, akalipokea mara kwa furaha;
21. lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa.

Yohana 8:31-32
31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;
32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.

Yohana 10:28-29
28. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.
29. Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.

Yohana 16:8
Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.

Warumi 8:28
Bende wang'eyo ni e gik moko duto tiyo maber ne jogo mohere, jogo moselu-ongi kaluwore gi dwarone.

Warumi 8:35-39
35. Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
36. Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.
37. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
38. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,
39. wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Wafilipi 1:6
Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;

Wakolosai 1:21-23
21. Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa;
22. katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama;
23. mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake.

Waebrania 1:14
Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?

I Petro 1:5
Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.

I Yohana 2:19
Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.

16. Ya wenye Haki na Wasio Haki

Tunaamini ya kwamba kuna tofauti kubwa kati ya wenyehaki na wasiohaki; kwamba ni wale tu kwa imani walio hesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu na kutakaswa na Roho wa Mungu, hao ndio wenye haki kwa heshima yake kubwa; wakati wengine wote hawajali kuhusu dhambi zao na kutoamini kwao hao ndio wasio haki na hata waliokufa katika furaha ya milele ya wateule na kuteseka kwa milele kwa walio potea.


23 Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu?

Mithali 11:31
Behold, the righteous shall be recompensed in the earth: much more the wicked and the sinner.

Mithali 14:32
The wicked is driven away in his wickedness: but the righteous hath hope in his death.

Malachi 3:18
Then shall ye return, and discern between the righteous and the wicked, between him that serveth God and him that serveth him not.

Mathayo 7:13-14
13 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

Mathayo 25:34
Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

Luka 9:26
Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu.

Luka 16:25
Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.

Yohana 8:21
Basi akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta; nanyi mtakufa katika dhambi yenu; mimi niendako ninyi hamwezi kuja.

Yohana 12:25
Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele.

Matendo ya Mitume 10:34-35
34. Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;
35. bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.

Warumi 1:1
Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu;

Warumi 6:16-18
16. Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.
17. Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;
18. na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.

Warumi 6:23
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Warumi 7:6
Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko

I Wakorintho 15:22
Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.

Wagalatia 3:10
JKwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.

I Petro 4:18
Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi?

I Yohana 2:7
Wapenzi, siwaandikii amri mpya, ila amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Na hiyo amri ya zamani ni neno lile mlilolisikia.

I Yohana 2:29
Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye.

I Yohana 5:19
Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.

17. Ya Serikali

Tunaamini ya kwamba mamlaka imeamriwa na Mungu, kwa mipangilio mizuri ya Binadamu; kwamba maombi yanastahili kwa maahakimu, kupewa heshima na kuwatii, isipokuwa kwa mambo yale ambayo ni kinyume na mapenzi ya Bwana Yesu Kristo, Yule pekee ndio Bwana wa thamira, na mfalme wa wafalme ambaye yu aja duniani tena.

Kutoka 18:21-22
21 Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi;
22. nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe.

2 Samweli 23:3
Mungu wa Israeli alisema, Mwamba wa Israeli aliniambia, Atawalaye wanadamu kwa haki, Akitawala katika kicho cha Mungu,

Zaburi 72:11
Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie.

Daniel 3:17-18
17. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme.
18. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.

Mathayo 10:28
Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.

Mathayo 22:21
Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Akawaambia, Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.

Mathayo 23:10
Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo.

Matendo ya Mitume 4:19-20
19. Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe;
20. maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.

Matendo ya Mitume 23:5
Paulo akasema, Sikujua, ndugu zangu, ya kuwa yeye ni Kuhani Mkuu; maana imeandikwa, Usimnenee mabaya mkuu wa watu wako.

Warumi 13:7
Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.

Wafilipi 2:10-11
10. ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11. na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Tito 3:1
Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema;

I Petro 2:13-14
13. Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa;
14. ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema.

I Petro 2:17
Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.

18. Ya ufufuo na Kurudi kwa Kristo na Matokeo ya Baadaye

Tunaamini kwa kukubali maandiko takatifu yanayo yahusu mafundisho hayo vile yalivyo na maana yake kwa utimilifu. Ya ufufuo, tunaamini kimwili Kristo alifufuka “Siku ya tatu kulingana na maandiko”. Kwamba alipanda “akaketi mkono wa kuume wa Mungu” kwamba “yeye pekee ndiye kuhani wetu mkuu mwaminifu na mwenye Huruma kwa mambo yanayomuhusu Mungu,” Kwamba huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu Mbinguni, atakuja jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake Mbinguni,” Kimwili, yeye mwenyewe, na ataonekana; na kwamba nao “waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza”. Na kwamba wenye haki walio hai, waliosalia, watanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, kumlaki Bwana hewani. “Kwa daika moja, kufumba na kufumbua nasi tutabadilika wakati wa parapanda ya miwsho. Kwamba Bwana Mungu atampa yeye kiti cha ufalme cha Baba yake Daudi na kwamba Kristo atatawala miaka elfu na utakatifu mpaka pale atakapowaweka maadui wake chini ya miguu yake.

 • Kristo alikuja na akazaliwa na Bikira,
 • Aliishi bila dhambi.
 • Akashitakiwa na akapatikana na atia.
 • Wakamsulubisha msalabani ambapo alikufa kwa anjili ya dhambi zetu.
 • Siku tatu baadaye akafufuka.
 • Tunangoja kurudi kwake hewani.
 • Atanyakua juu Kanisa (Waamini)
 • Baadaye itakuwa miaka saba ya dhiki pamoja na shetani mkuu wa ulimwengu.
 • Yesu atarudi tena kwa Mlima wa Mungu na kuyashinda majeshi ya Mpinga Kristo katika vita vya Har-magedoni.
 • Kristo anaweka utawala wake miaka elfu moja.
Zaburi 72:8
Na awe na enzi toka bahari hata bahari, Toka Mto hata miisho ya dunia.

Isaya 11:4-5
4. bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.
5. Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia.

Mathayo 24:27
Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

Mathayo 24:42
Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.

Mathayo 28:6-7
6. Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa.
7. Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu. Tazama, awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha waambia.

Marko 16:9
Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba.

Luka 1:3
nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu,

Luka 24:2
Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi,

Luka 24:4-6
4. Ikawa walipokuwa wakifadhaika kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumeta-meta;
5. nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hata nchi, hao waliwaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu?
6. Hayupo hapa, amefufuka. Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa akaliko Galilaya,

Luka 24:39
Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.

Luka 24:51
Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni.

Yohana 14:3
Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.

Yohana 20:27
Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye.

Matendo ya Mitume 1:9
Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.

Matendo ya Mitume 1:11
wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.

I Wakorintho 15:4
na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;

Wafilipi 4:20
Sasa atukuzwe Mungu, Baba yetu, milele na milele. Amina.

I Wathesalonike 4:16
Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza

I Timotheo 2:5
Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;

Waebrania 2:17
Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.

Waebrania 5:9
naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;

Waebrania 8:1
Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,

Waebrania 9:28
kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.

Waebrania 12:2
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

19. Ya Umisheni

Umisheni ni kweli kwenda duniani kote kupeleka injili ya Yesu; alikufa, na akafufuka. Kuwabatiza katika jina la Baba, la Mwana na Ya Roho mtakatifu. Na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi, na kurudia kutenda hivyo tena na tena.

Mathayo 28:18-20
18. Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
19. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20. na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Marko 16:15
Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

Yohana 20:21
Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.br>
Matendo ya Mitume 1:8
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Warumi 10:13-15
13. kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.
14. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?
15. Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!

20. Nehema ya Kupeana

Kupeana kimaandiko ni moja baadhi ya misingi ya imani.

2 Wakorintho 8:7
Lakini kama mlivyo na wingi wa mambo yote; imani, na usemi, na elimu, na bidii yote, na upendo wenu kwetu sisi; basi vivyo hivyo mpate wingi wa neema hii pia.

I Wakorintho 16:2
Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;

Waebrania 7:2
ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;

Waebrania 7:4
Basi, angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambaye Ibrahimu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara.

Mathayo 23:23
Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.

We are commanded to bring the tithe into the common treasury of the church.

Leviticus 27:30
Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana.

Malachi 3:10
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

Matendo ya Mitume 4:3-35
3. Wakawakamata, wakawaweka gerezani hata asubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni.
4. Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano.
5. Hata asubuhi wakubwa na wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemu,
6. na Anasi Kuhani Mkuu, na Kayafa pia, na Yohana na Iskanda, na wote wale waliokuwa jamaa zake Kuhani Mkuu.
7. Walipowaweka katikati wakawauliza, Kwa nguvu gani na kwa jina la nani ninyi mmefanya haya?
8. Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli,
9. kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa,
10. jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu.
11. Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni.
12. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
13. Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.
14. Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu.
15. Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakafanya shauri wao kwa wao,
16. wakisema, Tuwafanyie nini watu hawa? Maana ni dhahiri kwa watu wote wakaao Yerusalemu ya kwamba ishara mashuhuri imefanywa nao, wala hatuwezi kuikana.
17. Lakini neno hili lisije likaenea katika watu, na tuwatishe wasiseme tena na mtu awaye yote kwa jina hili.
18. Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu.
19. Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe;
20. maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.
21. Nao walipokwisha kuwatisha tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu; kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka;
22. maana umri wake yule mtu aliyefanyiwa ishara hii ya kuponya ulipita miaka arobaini.
23. Hata walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha habari ya mambo yote waliyoambiwa na wakuu wa makuhani na wazee.
24. Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;
25. nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?
26. Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake.
27. Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,
28. ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee.
29. Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote,
30. ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.
31. Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.
32. Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.
33. Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote.
34. Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa,
35. wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji.

Matendo ya Mitume 4:37
alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume.

Open BIBLE to beat devil
AMAZING GRACE BIBLE INSTITUTE